LIVE STREAM ADS

Header Ads

TCRA YAOMBWA KUTOMINYA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI.

Getruda Ntakije na Judith Ferdinand
Chama cha waandishi wa habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania(OJADACT), kimeiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) isiminye uhuru wa vyombo vya habari  pamoja na haki ya wananchi  kupata taarifa, pia itazame utekelezaji wa sheria ya  maudhui ya utangazaji.

Hii imetokana na sheria hiyo kutokuwa rafiki kwa vyombo vya habari  huku ikilenga kuvibana  vyombo hivyo kutofanya kazi ipasavyo kuelekea uchaguzi mkuu  unaotarajia kufanyika mwezi oktoba mwaka huu, kama zilivyo sheria za makosa ya mtandaoni na takwimu zinazoanza kutumika septemba 1.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti  wa OJADACT, Edwin Soko  kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za chama hicho, zilizopo wilayani Nyamagana mkoani hapa.

Soko alisema, sheria hiyo ina mkinzano mkubwa na misingi ya  kitaaluma ya  tasnia hiyo kama kutotambua falsafa ya vyombo vya habari na mlengo wao, kutotaka kutambua kuwa mtu anaweza kutengeneza habari (prominence).

Aliongeza kwa kusema kuwa,  inadumaza uwezo wa mwandishi wakati wa mahojiano kwa kutofanya majadiliano mafupi ya hitimisho na uchambuzi wa hoja za wahojiwa mwishoni mwa kipindi.

“Sheria hii haijahusisha wadau wa habari na kwa namna moja au nyingine inakosa baraka za  wadau, jambo linalotia shaka na kuwa kati ya sheria zinazotungwa kwa lengo la kukomoa kundi fulani la kitaaluma,” alisema Soko.

Pia alisema kuwa, sheria hiyo   imeweka mitego mipana ya mambo ambayo hayatakiwi kama kifungu cha 15 (2) kinasema,  No Broadcast any politically – related matter which may reasonable upset the balance to be observed, hiyo ni wazi kuwa kuna  mkinzano wa maana pana inayoweza kutafsiriwa na mamlaka moja tu, yani watunga sheria na sio watumiaji wa sheria.

Aidha alisema kuwa, sheria hiyo imenyakua miongozo ya kitaaluma kwa mwandishi na kuifanya sheria  badala ya kuiacha katika maadili ya kitaaluma  ( Media ethics), ambayo ingeweza kusimamiwa  na vyombo  husika  kama MCT, UTPC, OJADACT, MISA, TAMWANA na vingine.

Hata hivyo aliiomba serikali iache kuwa na ajenda ya siri katika kuvibana vyombo vya habari wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu badala yake ishirikiane na vyombo hivyo kutengeneza  ajenda ya kuwavusha salama  watanzania kwenye uchaguzi huo.

No comments:

Powered by Blogger.