LIVE STREAM ADS

Header Ads

BANDARI YA NCHI KAVU ISAKA WILAYANI KAHAMA KUANZA KAZI MWEZI MWEZI SEPTEMBA MWAKA HUU.

Na:Shaban Njia
Bandari ya Isaka iliyopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga haijahamishwa kwenda Mjini Shinyanga kama inavyodhaniwa bali ilisimama kutokana na kuharibika kwa Miundombinu ya Reli na Mabehewa iliyokuwa katika eneo hilo.

Jana Mkuu wa bandari hiyo Ramadhan Gumbo alisema mabehewa mengi yalikuwa hayana uwezo wa kusafirisha abiria na mambo mengine  hivyo sasa jitihada zimefanyika ya kurudisha hali ya zamani.

Alisema tayari kuna matengenezo yanafanyika ili kuwa na usafiri wa uhakika na kwamba bandari hiyo itarejea  mapema mwezi wa tisa  au mwishoni mwa mwezi huo na kutoa huduma kama ilivyo kuwa hapo awali.

"Watu wanasema bandari ya Isaka imekufa eti imehamishwa na kwenda Mjini Shinyanga,hayo si kweli bali kulikuwa na matengenezo ya kuboresha huduma na sasa kufikia mwezi wa tisa mwanzoni au mwishoni reli itaanza kutumia kama miaka ya nyuma"alisema.

Aliwataka wananchi kuwa tayari kutumia usafiri huo ambao utakuwa ukitumia siku mojakwenda Jijini Dar Es Salaam kutoka Shinyanga.

Katika hatua nyingine Wafanyakazi wanaofanyakazi ya ulinzi wa kamapuni ya Integrated Security System Limited inayotoa huduma ya ulinzi  katika Shirika la reli  nchini katika bandari hiyo wamemuomba waziri wa uchukuzi Samweli Sitta kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kucheleweshewa mishahara kufanya kazi bila mikataba.

Wafanyakazi hao walisema kuwa malalamiko yao makubwa ni kutopewa mikataba ya kazi tangu mwaka 2013 mpaka sasa na kutoingizwa katika mifuko ya jamii madai ambayo Kampuni hiyo haijayafanyia kazi kwa mda mrefu licha ya kuwasilisha malalamiko yao.

Walisema kampuni hiyo imekuwa ikiwacheleweshea mshahara kwa zaidi  ya miezi miwili hadi mitatu hali amabyo inawaanya wengine washindwe kumudu gharaa ya maisha.

No comments:

Powered by Blogger.