CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI MWANZA CHAENDELEA KUWANADI WAGOMBEA WAKE.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Chama hicho jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula (Kulia).
Na:George GB Pazzo
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza
Wikendi hii kimeendelea kuwanadi Wagombea wa nafasi za Uongozi katika ngazi ya
Udiwani, Ubunge na Urais kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara.
Katika
Mikutano hiyo, Katibu wa chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu anawahimiza
Wananchi kuwachagua viongozi bora kwa ajili ya maendeleo yao na kuachana na
baadhi ya wagombea wenye nia ya kuvuruga amani ya Taifa ambao wanaomba uongozi
kwa majaribio.
Kiswaga
Boniventura Destery ni mgombea Ubunge wa CCM kutoka Jimbo la Magu, katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama
hicho katika jimbo hilo uliofanyika juzi jumamosi alisema kuwa matatizo ya wanamagu anayajua hivyo wamchague awe mbunge wao kwa ajili ya kuishinikiza Serikali kwa ajili ya kuyatatu na kuongeza kuwa kero ya Maji katika jimbo hilo sasa inakwenda kufikia mwisho.
Akiwahutubia
wakazi wa Kata ya Buhongwa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana,
Stanslaus Mabula ambae ni Mgombea Ubunge Jimbo la Nyamagana aliwaomba wananchi kumpa ridhaa ya kuwa mbunge wao ili aweze kushirikiana nao katika kuwaletea maendeleo katika sekta za elimu, afya, maji, umeme, miundombinu pamoja na kuondoa kero za ardhi Jijini Mwanza.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA RIPOTI KAMILI
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akimnadi Mgombea Ubunge wa chama hicho Jimbo la Magu Kiswaga Boniventura Destery (kulia).
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya kutoka Chama cha Mapinduzi CCM Baraka Konisaga akisalimia katika Mkutano wa kuwanadi wagombea jimbo la Nyamagana uliofanyika jana katika Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wa CCM Mkoani Mwanza
Wananchi na Makada wa CCM Wakifuatilia Mkutano wa CCM uliofanyika jana katika Kata ya Buhongwa
No comments: