LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAHAFARI YA CHUO CHA UVUVI NYEGEZI JIJINI MWANZA YAFANA. WIZARA YATOA TAHADHARI KWA WAVUVI.

Judith Ferdinand
Kaimu Mkurungezi wa wizara ya mifugo na uvuvi nchini Simba Liganga amewataka Wavuvi wa samaki walioka kanda ya ziwa kufuata kanuni na taratibu za uvuvi zilizowekwa na serikali katika kumvua samaki mwenye uzito uliopangwa na serikali.

Akizungumza juzi katika mahafari ya nne ya chuo cha uvuvi kampasi ya Nyegezi Jijini Mwanza, Liganga alisema wavuvi walio wengi hawazingatii sheria na taratibu zilizowekwa na serikali na kwamba wengi wao hutumia dhana haramu.

Alisema endapo wavuvi hao watazingatia taratibu na sheria za uvuvi, sekta hii itaweza kuongeza pato la taifa kwa asilimia kubwa ukilinganisha na sasa ambapo huongeza asilimia 2, huku asilimia 10 huingiza pesa za kigeni.

“Bado tunachangamoto kubwa katika sekta ya uvuvi ambapo wavuvi wengi wanataumia dhana hatarishi katika kujipatia samaki, na wengine huvua samaki ambao hawajafikia kiwango cha kuvuliwa, uvuvi wa namna hii utafanya maziwa yetu yapungukiwe na samaki kwa asilimia kubwa, hivyo nawomba wavuvi wote kuzingatia sheria za uvuvi zilizowekwa na serikali”alisema Liganga.

Aidha, Liganga alisema kutokana na hali halisi ilivyo nchini, serikali na asasi zisizo za kiserikali hazijawa na ajira za kutosha kuweza kuajiri watu wengi wanaohitimu vyuo, hivyo jambo la kujiajiri kwa kufuta taratibu za ufugaji wa samaki kwa kuchimba mabwawa ukizingatiwa kwa ufanisi utaweza kuwapatia ajira zao binafsi.

Pia alisema, zao la samaki limetokewa kupendwa na watu wengi kwasababu lina lishe bora kuliko zao la nyama nyekundu ambalo kwa kiasi kikubwa wataalamu wa afya hawawashauri kutumia, hivyo wananchi hawanabudi kuanzisha ajira zao binafsi kwa kuanzisha ufuagi wa samaki.

Mtendaji Mkuu wa Uvuvi nchini Yahya Ibrahim alisema, kwa sasa upatikanaji samaki katika vyanzo vya asili umepungua kwa asimilia kubwa, kutokana na hali hiyo wameamua kuanzisha mafunzo kwa vijana hasa wakijijini jinsi ya kufuga samaki.

Alisema mpaka sasa wameenda mbali zaidi katika utoaji wa elimu kwa kuanza kuwafundisha wafanyakazi wa viwanda vya kusindika samaki vilivyopo Kanda ya Ziwa jinsi ya kuwatunza samaki wasiweze kuharibika mapema.

Alisema, pia wanajitahidi kutoa elimu na kuwahamasiha wananchi kuhusiana na ufugaji wa samaki na namna ya kuwatunza hadi kufikia kiwango cha kuvuliwa.

Awali akisoma hotuba kwa mgeni rasimi Mkurungezi wa chuo cha Nyegezi Charles Swai alisema, mahafali hayo ni 35 tangu kuanzishwe kwa chuo cha uvuvi nchini, na ya nne chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Uvuvi (FETA), hivyo kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya  ukosefu wa usafiri, maktaba za kujifunzia, vifaa vya kufundishia na kupatiwa muda  mdogo wa mafunzo(FIELD).

Hata hivyo jumla ya wanafunzi 251 wamehitimu mafunzo katika ngazi ya  Astashaha na stashada kwa kozi za sayansi na teknolojia ya uvuvi, usimamizi wa rasilimali pamoja na ufundi wa majokofu na viyoyozi.

No comments:

Powered by Blogger.