LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YAZIDI KUONGEZEKA KATIKA KAHAMA.

Na:Shaban Njia
Imeelezwa Kuwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga bado yako katika kiwango cha juu baada ya watu 18 kati ya 341 waliopima afya zao kubainika kuwa na maambukizi hayo.

Hayo yalibainishwa juzi na mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya wakati akisoma taarifa fupi ya watu waliojitokeza kupima afya zao kwa hiari siku ya mkesha wa mwenge uliofanyika katika viwanja vya Kagongwa. 

Aidha Mpesya alifafanua kuwa kati ya watu 341 waliojitokeza kupima afya zao, wanaume ni 209 na wanawake wakiwa 132 na kusema kati ya idadi hiyo kati yao waliokutwa na maambukizi, wanaume ni wawili na wanawake 16 na kuongeza kuwa kiwango hicho ni sawa na asilimia 5.3.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Juma Khatibu Chum aliwataka wananchi kulichukulia suala hilo kama janga la kitaifa na kuwataka wananchi pamoja na familia zao kutowanyanyapaa hivyo washirikiane nao katika shughuli za kimaendeleo.

Katika mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 kauli mbiu inasema ”tumia haki yako, jiandikishe na tumia haki yako ya kidemokrasia kupiga kura 2015". 

No comments:

Powered by Blogger.