TANZANIA KUPOKEA ZAIDI YA DOLA MILIONI MOJA KWA AJILI YA KUFIKISHA UMEME KOTE NCHINI.
Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi tano barani Afrika zitakazopokea ongezeko la dola milioni 1.1 kutoka Serikali ya Marekani kwa ajili ya kuboresha shughuli za uzalishaji wa nishati ya umeme ili uweze kuyafikia maeneo
mengi zaidi nchini ambayo hayapo katika Gridi ya Taifa.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Marekani inayoshughulikia maendeleo kwa Bara la Afrika USADF na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani USAID Nchi nyingine zitakazonufaika ni Kenya, Nigeria, Ghana na Ethiopia.
Taasisi hiyo imesema kupitia mpango huo jumla ya kampuni 11 kutoka nchi hizo Tano zitapokea msaada wa hadi Dola 100,000 za Marekani ambao ulitangazwa na Rais wa Marekani Barack Obama alipohutubia Mkutano wa Mwaka wa Kimataifa wa wajasiriamali uliofanyika nchini Kenya.
Wakati Mipango ikiwa hivyo, bado watanzania katika maeneo mbambali yaliyofikiwa na Umeme, wanazidi kulalamika kutokana na ukosefu wa umeme wa uhakika hususani katika kipindi hiki ambacho imeelezwa kuwa umeme utakuwa ukikatika mara kwa mara kutokana na matengenezo na majaribio ya mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi asilia.
Kwa Hisani Ya Mtandao

No comments: