LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATAKIWA KUONDOA NA KUDHIBITI GUGUMAJI KATIKA KINGO ZA ZIWA VICTORIA MKAONI MWANZA.

Zoezi la uondoaji wa gugumaji katika eneo la Nera Jijini Mwanza linalofanywa na Kikundi cha kudhibiti rasirimali za Ziwa Victoria kutoka Kata ya Kirumba likifanyika leo.
Na:George GB Pazzo
Wamiliki wa Vyombo vya Majini pamoja na Waendeshaji wa Shughuli mbalimbali za uzalishaji katika maeneo ya kingo za Ziwa Victoria Mkoani Mwanza, Wametakiwa kusaidia katika kutokomeza gugumaji linayozidi kusambaa katika ziwa hilo.

Kauli hiyo ilitolewa mapema leo na Mwenyekiti wa Vikundi vya Wavuvi Vinavyosimamia rasirimali za Ziwa hilo (BMU) Kata ya Kirumba Wilayani Ilemela Costantin John Mnyere wakati wa zoezi la kuondoa gugumaji katika eneo la Nera Jijini Mwanza.

Alisema kuwa wamiliki wa vyombo vya majini ikiwemo Meli, feri pamoja na wazalishaji wa shughuli za kilimo pembezoni mwa ziwa Victoria, wanapaswa kusaidia katika uondoaji na udhibiti wa gugumaji katika kingo za maeneo yao badala ya kusubiri juhudi pekee za kupambana na gugumaji zinazofanywa na Vikundi vya BMU.


Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti wa gugumaji Kata ya Kirumba Jane Misso alisema kuwa pia Viongozi wa Serikali wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri wanapaswa kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wananchi kuwa mstari wa mbele katika kupambana na gugumaji hususani wanayoendesha shughuli za kilimo cha mbogamboga.

Hata hivyo uongozi wa Soko Kuu la Samaki Kirumba umepongezwa kwa namna unavyosaidia katika kuondoa na kupambana na gugumaji katika kingo zilizopo katika Soko hilo ambapo wadau wengine wamehimizwa kuigwa mfano huo.

Zoezi la uondoaji wa gugumaji katika eneo la Nera Jijini Mwanza linalofanywa na Kikundi cha kudhibiti rasirimali za Ziwa Victoria kutoka Kata ya Kirumba likifanyika leo.
Zoezi la uondoaji wa gugumaji katika eneo la Nera Jijini Mwanza linalofanywa na Kikundi cha kudhibiti rasirimali za Ziwa Victoria kutoka Kata ya Kirumba likifanyika leo.
Kulia ni Mwenyekiti wa Vikundi vya Wavuvi Vinavyosimamia rasirimali za Ziwa hilo (BMU) Kata ya Kirumba Wilayani Ilemela Costantin John Mnyere akizungumza na Gwido the Best kutoka Radio Metro Fm (Kushoto).
Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti wa gugumaji Kata ya Kirumba Jane Misso akizungumza na Gwido the Best kutoka Radio Metro Fm (Kushoto).

No comments:

Powered by Blogger.