LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAGUENI VIONGOZI WATAKAOENDELEZA UJENZI WA MAABARA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI.

Na:Shaban Njia
Watanzania wametakiwa kuchagua viongozi wenye Uchungu na Elimu watakaojali na kuendeleza ujenzi wa Maabara katika shule za Sekondari za kata kwa lengo la kukuza Elimu kwa Wanafunzi sambamba na kupunguza Vijana tegemezi.

Hayo yalisemwa juzi na mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa Hassan Hakimu wakati wa ufunguzi wa kuweka jiwe la msingi katika maabara ya sekondari ya kata ya Kinaga iliyojengwa kwa nguvu ya halmashauri ya mji wa Kahama Mkoani Shinyanga na kampuni ya ACACIA Kupitia mgodi wake wa dhahabu Buzwagi.

Awali akisoma taarifa ya shule hiyo ya ujenzi wa maabara hiyo Mkuu wa shule Agines Katabalwa alisema kuwa ujenzi wa maabara umegharimu kias cha shilling Millioni 200 huku halmashauri ya mji ikitoa kiasi cha shilling Millioni 40 na mgodi wa Buzwagi ukitoa Millioni 160.

Katabalwa alisema kuwa ukamilikaji wa maabara hiyo utasaidia wanafunzi kusoma kwa bidii masomo ya sayansi na ukizingatia kuwa maabara hiyo imekamilika ikiwa na vifaa vyote vinavyohusika na masoma ya sayansi,kama vile Fizikia,Bailojia pamoja na Kemia.

Kwaupande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya alisema kuwa ukamilishaji wa ujenzi wa maabara ni mahusiano mazuri kati ya serikali na wawekezaji hali ambayo imeonesha kuwepo kwa matunda mazuri kama vile ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara kwa wakati.

“Wawekezaji sio watu wabaya,mkikaa mezani na ukatoa matatizo yako ambayo hayagusi faida yao kubwa ambayo wanayoipata katika shughuri zao za uchimbaji unaweza kusaidia,kuliko kuomba kitu kikubwa ambapo kinaweza kuwaathiri katika uzalishaji wao kwani wametumia mtaji mkubwa katika kuwekeza". Alisema Mpesya na kuongeza;

“Kwa upande wa halmashauri ya mji hatuwezi kuipongeza kwani ni jukum lao katika kuchangia masuala yote ya maendeleo katika halmashauri husika,kwaleo serikali inampongeza mwekezaji kwa kusikia kilio chetu cha kuwakomboa wanafunzi na kuwasaidia katika masomo ya sayansi”.

Hata hivyo mkimbiza mwenge huyo alisisitiza kwa  serikali kuwa karibu na wawekezaji na kushirikiana katika masuala mbalimbali ya maendeleo hali ambayo inaweza kusaidia kuleta maendeleo ya haraka katika maeneo husika.

Kwaupande wake mwalimu wa masomo ya sayansi katika mshule hiyo Jakison Kwilasa alisema kuwa anafarijika kuwa na maabara ya kisasa ambayo haijapungukiwa na vitendea kazi vya kufanyia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi hali ambayo inaweza kuchangia kuleta ufaulu mkubwa katika masomo ya sayansi katika shule za sekondali za kata.

Katika mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 kauli mbiu inasema ”tumia haki yako, jiandikishe na tumia haki yako ya kidemokrasia kupiga kura 2015. 

Mwenge huo umemaliza mbio zake jana katika halmashauri mji wa Kahama ambapo ulizindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Billioni 1.4 na kukabidhiwa katika manispaa ya Shinyanga.

No comments:

Powered by Blogger.