LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWAUASA YALALAMIKIWA KUTODHIBITI MIFUMO YAKE YA MAJITAKA JIJINI MWANZA. HUDUMA ZAFUNGWA.

Miundimbinu ya Majitaka ilivyo katika eneo la Furahisha
Na:George GB Pazzo
Mamlaka ya Majitaka na Majisafi Mkoani Mwanza Mwauasa imetakiwa imelalamikiwa kutokana na mifumo yake ya majitaka kuziba mara kwa mara katika maeneo mbalimbali na hivyo kusababisha adha kubwa kwa wananchi.

Wananchi pamoja na Wajasiriamali katika eneo la Furahisha Jijini Mwanza jana walitoa malalamiko hayo baada ya miundombinu ya majitaka katika eneo hilo kuziba kwa takiribani wiki moja sasa huku Mwauasa ikishindwa kuchukua hatua za haraka ili kuondoa hali hiyo.

Waliiomba Mwauasa kuzibua miundombinu hiyo ili kuondoa hatari ya magonjwa ya milipuko inayoweza kujitokeza ikizingatiwa kuwa shughuli mbalimbali zinafanyika katika eneo hilo ikiwemo za chakula zinazofanywa na mamantilie.

Msimamizi wa Mradi wa huduma za bafu na choo uliopo katika Uwanja wa Furahisha Jane Misso alisema kuwa hali hiyo imesababisha mradi huo kufungwa ambapo ameomba hatua za haraka kuchukuliwa ili kuondoa kero hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu, Afisa Uhusiano wa Mwauasa Robert Masunya aliahidi kufuatilia malalamiko hayo kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.
Mradi huu wa choo na bafu katika eneo la furahishwa umefungwa kutokana na mfumo wa majitaka unaopaswa kwenda katika maeneo ya kukusanyia majitaka kuziba na hivyo majitaka hayo kupitia katika mifereji ya mradi huu na kutiririka hadi ziwani.
Mradi huu wa choo na bafu katika eneo la furahishwa umefungwa kutokana na mfumo wa majitaka unaopaswa kwenda katika maeneo ya kukusanyia majitaka kuziba na hivyo majitaka hayo kupitia katika mifereji ya mradi huu na kutiririka hadi ziwani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti wa gugu maji Kirumba Kati Jane Misso akijionea hali ilivyo
Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti wa gugu maji Kirumba Kati Jane Misso akijionea hali ilivyo
Kamera ya Binagi Media Group na Mic ya Radio Metro ilimkuta kijana Yohana Samweli ambae ni Machinga akibeba udongo kwa ajili ya kwenda kumwaga katika eneo lake la kazi baada ya majitaka kutuama katika eneo hilo.
Mzee Malima Makoba akitoa malalamiko yake kupitia Metro Fm ambapo aliihimiza Mwauasa kutoka maofisini ili kutatua kero zinazosababishwa na miundombinu yake.
Mtaani kuko hivi baada ya Mifumo mbalimbali ya Majitaka kuziba Jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.