LIVE STREAM ADS

Header Ads

INASIKITISHA SANA. KIJANA HUYU ANAPITIA MATESO MAKUBWA. ONYESHA MOYO WAKO WA HURUMA.

Na:George GB Pazzo
Kijana Josephat Emmanuel (20) Mkazi wa Nata Jijini Mwanza amejitokeza hadharani na kuomba ufadhiri wa Watanzania, ili aweze kupata matibabu ya kuwekewa jicho bandia pamoja na miwani baada ya jicho lake kuharibika.

Akizungumza na Radio Metro jana, Emmanuel alisema kuwa alizaliwa Mwaka 1995 Wilayani Sengerema akiwa na ulemavu wa jicho la kushoto ambalo lilipelekea kushindwa kuendelea na masomo yake na hivyo kuishia darasa la tano. 

"Niliteseka sana tangu nilipozaliwa hadi mwaka jana nilipopata msaada wa wasamalia wema na hivyo kuanza matibabu katika Hospitali ya Mission Sengerema. Huko nikaambiwa napaswa kusafirishwa hadi Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu kwa kuwa wao hawawezi kunitibu maana tatizo lilikuwa kubwa". Alisema Emmanuel na kuongeza;

"Nilipofika Bugando napo nikaambiwa tatizo langu ni kubwa hivyo napaswa kupelekwa katika Hospital ya Taifa Mhimbili Jijini Dar es salaam ambapo wasamalia wema pia walinichangia pesa na hivyo kufanikiwa kufanyiwa oparesheni". Alieleza Emmanuel.

Alisema baada ya oparesheni hiyo alipewa ushauri wa kitaalamu kuwa anapaswa kuwa anafika Mhimbili kila baada ya miezi sita kwa ajili ya kusafishwa jicho hilo huku akitakiwa kuwekewa jicho bandia pamoja na kuwa na miwani ya macho.

"Niliambiwa nilipie gharama za jicho bandia pamoja na pesa ya miwani lakini kwa sababu pesa nilikuwa nimemaliza, niliamua kurudi nyumbani hadi sasa ambapo nimejitokeza tena ili wasamalia wema wanisaidie pesa ili nipate huduma hizo". Alifafanua Emmanuel.

Emmanuel alitanabaisha kuwa kwa sasa anaishi na bibi yake jijini Mwanza na kwamba mama yake alifariki mwaka 2004 huku akiwa hajui baba yake alipo japo anasikia kuwa yuko katika visiwa vya ukerewe Mkoani Mwanza.

Wasiliana na bibi yake na kijana Emmanuel kwa nambari 0763 063 631 ikiwa umeguswa kumsaidia ili kuondokana na adha anayoipata kutokana na tatizo linalomsibu.

No comments:

Powered by Blogger.