LIVE STREAM ADS

Header Ads

AUAWA KWA MAPANGA BAADA YA MME WAKE KUOA MKE WA PILI.

Na:Raymond Mihayo
Mama mmoja mkazi wa kijiji cha Kabondo kata ya Mwanase wilayani Kahama Mkoani shinyanga ameuawa kwa kukatwa mapanga kutokana na mgogoro ya kifamilia.

Kamanda wa polisi Mkoa wa shinyanga Justus Kamugisha alimtaja mama huyo aliyeuawa kuwa ni Mwalu Makoye (35) aliyeuawa kutokana na kudai sehemu ya mali ya familia baada ya mumewe kuoa mke mwingine.

Akielezea tukio hilo Kamugisha alisema kuwa mwanamke huyo aliuwawa kwa kukatwa mapanga eneo la begani na kwamba mtuhumiwa mmoja aitwae Simon Busungu ambae ni mme wa marehemu anashikiriwa na polisi kutokana na kuhusishwa na mauwaji hayo.

No comments:

Powered by Blogger.