LIVE STREAM ADS

Header Ads

ELIMU BADO INAHITAJIKA ILI KUTOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO NA VIKONGWE MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia,Kahama
Pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali kukomesha mauwaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi(ALBINO) lakini bado elimu inatakiwa kutolewa zaidi hasa mashuleni hali ambayo inaweza kupunguza wingi wa mauaji hayo hasa katika Mkoa wa Shinyanga.

Kauli hiyo ilitolewa wiki hii na Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha wakati akizungumza na wazazi katika mahafari ya 11 ya wahitimu elimu ya msingi katika shule ya Rocken Hill Academy iliyopo mjini hapa.

Kamugisha alisema endapo elimu itatolewa kwa wingi hasa kwa wananfunzi inaweza ikawa msaada mkubwa nao kutoa elimu kwa wazazi wao hasa katika kipindi hiki wapo nyumbani kusubili kuendelea na masomo ngazi ya Sekondari hali ambayo inaweza ikawa mabadiliko hususani katika jamii inayowazunguka.

“Ndugu wanafunzi elimu mliyoipata kwa muda wa miaka saba muitumie vizuri kuwaelimisha wazazi na jamii hii inayowazunguka juu ya ukatili ya mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na vikongwe na kwamba watu wa aina hiyo ni binadamu kama tulivyo sisi, hawapaswi kunyanyaswa wala kufanyiwa vitendo vya ukatili kama mauaji”. Alisema Kamugisha.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Rocken Hill Academy Alexander Kazimiri aliwataka wahitimu hao wanaomaliza darasa la saba hapa nchini kusoma kwa bidii katika Elimu ya juu huku wakiwa na ndoto za maisha yao ya baadaye hali ambayo itaweza kuwasaidia pindi wanapoanza maisha ya kijitegemea pamoja na wazazi wao.

Kazimiri alisema kuwa kazi ya kusoma ni pale unapokuwa na maono ya baadaye ya maisha ikiwa ni sambamba na kusimamia nidhamu unapokuwa shuleni na kusikiliza mafunzo kutoka kwa Walimu   hali ambayo inaweza kuleta mafanikio makubwa katika maisha.

“Wazazi kazaneni kusomesha watoto wenu kwani elimu ya watoto wenu ni Bima ya uzeeni itakayowasaidia kuwatunza ninyi hivyo endeleeni kuwekeza katika suala la elimu katika kipindi hiki cha mapinduzi ya Sayansi na Teknolojia pia kama unataka kuwa Mhandisi lazima upende kusoma masomo ya Sayansi kama vile Phizikia, Bailogia pamoja na Kemia hali ambayo inaweza kukusaidia katika kufikia lengo la maisha yako ya baadaye”. Alisema Alexander Kazimiri Mkurugenzi wa Shule ya Rocken Hill Academy.

Mkurugenzi huyo aliwataka Wazazi wa watoto wanaohitimu Elimu hiyo ya Msingi kujua kuwa Wanafunzi ndio bima yao ya uzeeni na kupitia kwao wanaweza kuona matunda yake pindi wanapofanya vizuri katika masomo yao hali ambayo wanaweza kuona mafanikio pindi wanapopata kazi nzuri na kuweza kuwasadia.

No comments:

Powered by Blogger.