LIVE STREAM ADS

Header Ads

JESHI LA POLISI MKOANI SHINYANGA LAKAMATA MENO YA TEMBO.

Na Raymond Mihayo, Kahama
JESHI la polisi Mkoani Shinyanga linawashikilia watu wawili baada ya kuwakamata wakiwa na nyara za serikali (meno ya tembo) vipande 14 wakiwa njiani kutoka katika kijiji cha Ulowa kwenda kuviuza Kaliuwa Mkoani Tabora.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa shinyanga Justus Kamugisha alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa juzi majira ya saa sita mchana maeneo ya kijiji cha Ulowa katika halmashauri ya ushetu wakijiandaa kwenda kuuza meno hayo Mkoan Tabora.

Kamanda kamugisha aliwataja watuhumiwa hao wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni  Godfrey  Alex mkazi wa kata ya Ulowa wilaya ya Kahama  pamoja na  Juma Nkuli mkazi wa wilaya ya Kaliuwa mkoani Tabora.

Kamanda kamugisha alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa baada ya kupatiwa taarifa na wasamaria wema kwamba kulikuwa na watu wameonekana kuwa na pembe za Ndovu ambapo jeshi la polisi liliweka mtego hali iliyopelekea kuwakamata watu hao kirahisi.

Alisema kuwa baada ya kupata taarifa jeshi walijipanga na kuweka mtego kwa kujifanya niwanunuzi na ndipo walipofanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja huku mwingine akikimbia hali ambayo iliwapa urahisi polisi kukamata mzigo huo.

Mmoja wa watuhumiwa aliekimbia, alikimbizwa na wananchi na ndipo alipojisalimisha katika ofisi ya mtendaji wa kata hali ambayo ilirahisishia jeshi la polis kumtia mbaroni.

“Jeshi la polisi wilayani hapa halijawahi kukamata pembe za Ndovu nyingi kiasi hicho na kwamba tukio hilo ni la pili, mara nyingi zinazokamatwa hazihusishwi na pembe za ndovu nyingi pia hukamatwa kwa waganga wajadi ambapo huhusishwa na imani za kishirikina”. Alisema Kamugisha.

Hata hivyo alisema kuwa  kutokana na pembe za Ndovu zilizokamatwa inaonekana kuwa ndovu waliouwawa wako saba  huku jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi ili kuhakikisha kuwa  mtandao wa majangili hao unakamatwa mara moja.

No comments:

Powered by Blogger.