LIVE STREAM ADS

Header Ads

CCM ILEMELA YAZINDUA KAMPENI ZAKE ZA UCHAGUZI. MAMA MABULA AAHIDI KUSIMAMIA VYEMA ILANI.

Judith Ferdinand na Getruda Ntakije
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ilemela kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Angelina Mabula, amewaahidi wakazi jimboni humo, kusimamia na kutekeleza ilani ya chama hicho yenye lengo la kuleta maendeleo nchini ikiwa atashinda katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za kuwanadi na kuwatambulisha wagombea ubunge na udiwani wa jimbo hilo, uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Buswelu, mkoani hapa.

Alisema yeye si mgeni wa kazi anacheza namba sita hivyo atahakikisha anasimamia sera ya nchi kuhusu kila kata kuwa na zahanati, ili kumaliza tatizo la vifo vya watoto chini ya umri wa maiaka mitano na mama wajawazito vinavyotokea wakati wa kujifungua.

Pia alibainisha kuwa atahakikisha wazee wanapatiwa vitambulisho kwa ajili ya kupatiwa matibabu bila kuchangia gharama yoyote, sambamba na mifuko ya hifadhi ya jamii kuwafikia kila mmoja.

Hata hivyo alisema kuwa kutokana na sera ya chama hicho, kuwawezesha wananchi wa makundi yote, ataliangalia kundi la walemavu na vijana kwa kuwafundisha ujasiriamali na kuwawezesha  kupata mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Aliongeza kuwa uongozi hautaki mabavu hivyo atasimamia na kutekeleza ilani ya chama hicho kwa kuhakikisha miundombinu ya jimbo hilo, inafanyiwa marekebisho na kuwa katika kiwango kinachokubalika.

Katibu wa CCM Mkoani Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu aliwataka wananchi kuchagua viongozi waadilifu, wachapakazi  na waaminifu, ili kuleta maendeleo ya nchi ambao wanatokana na chama hicho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mwanza, Anthony Dialo aliwaomba viongozi wa dini kuwaruhusu waumini wao kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu ili wasikose fursa ya kuchelewa kupiga kura kama ilivyokuwa mwaka 2010.

No comments:

Powered by Blogger.