LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHABAINISHA AINA YA VIONGOZI WANAOHITAJIKA NCHINI.

Mgombea Ubunge wa Chama cha Alliance For Change and Transparency ACT Wazalendo katika Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza Mkiwa Adam Kimwanga (Kushoto) akiwa pamoja na Meneja Kampeni wake Pendo Ojijo (Kulia)
Na:George GB Pazzo
Chama cha Alliance For Change and Transparency ACT Wazalendo Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kimewataka Watanzania kuwachagua Viongozi watakaoisimamia Tanzania katika misingi ya Utu, Uzalendo pamoja na Uadilifu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Agost 25 mwaka huu.

Hayo yalisemwa juzi Mgombea Ubunge wa Chama hicho katika Jimbo la Ilemela Mkiwa Adam Kimwanga alipokuwa akiomba kura kwa wakazi wa Kata ya Nyamanoro jimboni humo na kuongeza kuwa ACT Wazalendo ndicho chama pekee nchini chenye viongozi wa aina hiyo.

Kimwanga ambae kwa awamu zote mbili za uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza kupitia Chama cha Wananchi CUF kabla ya kuhamia ACT Wazalendo alibainisha kuwa akipata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha anasimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo kutatua kero ya Maji, kukamilisha ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ilemela, kushughulikia kero na changamoto za elimu pamoja na kuwawezesha akina mama na vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia ajira shirikishi.

No comments:

Powered by Blogger.