JUMAC YAANDAA CHAKULA CHA HISANI JIJINI MWANZA KUSAKA MILIONI 200.
Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Watoto Yatima (JUMAC) wakiwa katika Mkutano na Wanahabari Jijini Mwanza.
Na:George GB Pazzo
Jumuiya ya Maendeleo ya Watoto Yatima Zanzibar JUMAC
inatarajia kuendesha harambee Jijini Mwanza kwa malengo ya kuchangisha fedha ili
kusaidia katika kukamilisha ujenzi wa shule na zahanati kwa ajili ya watoto
wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi wakiwemo yatima na wenye
ualibino katika Mji wa Pemba Zanzibar.
Hayo yalibainishwa jana na Mratibu wa Jumuiya hiyo Joseph
Sinde Magutu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza kuhusiana
na harambee hiyo na kuongeza kuwa matarajio ni kukusanya zaidi ya shilingi
milioni 200 zitakazosaidia kufikia malengo hayo.
Magutu alibainisha kuwa JUMAC kwa kushirikiana na
Chama cha Albino Mkoa wa Mwanza imeandaa chakula cha hisani ili kukamilisha
harambee hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika kesho katika Ukumbi wa Gold Crest
Hotel kuanzia majira saa moja jioni.
Wadau mbalimbali wakiwemo Wananchi, mashirika pamoja
na taasisi za serikali na binafsi wanaombwa kushiriki katika harambee hiyo
ili kusaidikia kufikia malengo yake ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo.
Katibu wa JUMAC Joseph Sinde Mabutu
Kaimu Mwenyekiti wa JUMAC Ramadhan Issa Kipaya
Amuru Abdallah Juma kutoka JUMAC
Mkutano wa Viongozi wa JUMAC na Wanahabari Jijini Mwanza
No comments: