SEHEMU YA KWANZA: HATUA SITA MUHIMU MTU ANAZOTAKIWA KUPITIA ILI KUFANIKIWA.
1.KUAMUA
Nipo na kamusi yangu nayoipenda ya webster na inasema kuamua ni chaguo ambalo mtu analifanya kuhusiana na kitu fulani baada ya kufikiri kwa kina kuhusiana na hicho kitu.
Kwa maana hiyo basi kuamua kunakuja baada ya mtu kufikiri kwa kina kuhusiana na jambo fulani, Sasa usije ukafanya uamuzi wowote kwenye maisha yako kama haujafikiri kwa kina maana mwisho wake utajuta na utagubikwa na huzuni.
Kuna kipindi nilikuambia kwamba tunafikiri kwa picha na pasipo picha kuna hali ya utatanishi katika akili. Nikitamka neno friji kinachokuja kwenye akili yako ni picha ya friji, kuku ni picha kadhalika, je gari lako ni picha pia je nikisema baba,mama,dada,kaka, lami,meza umeonaa eeeeeh picha za hivi vitu ndio zinakuja kwenye akili yako. Hivyo basi baada ya mtu kupata picha fulani kwenye akili yake sasa ndipo anapoamua kuhusu kitu kile.
Kwa sababu hiyo basi kuwa na tabia ya kupiga picha katika kila kitu unachokifanya, Mwalimu wangu Jihn Rohn alikuwa akisema mara kadhaa picha zinabeba maneno 1000
Siku ambayo umeamua kuhusu jambo fulani itakuwa ni siku nzuri sana katika maisha yako, lakini unatakiwa kufahamu kwamba ule motisha wa kuamua juu ya kitu fulani huwa unakaa kwa muda mfupi kama usipoenda hatua nyingine ambayo ni kupanga namna utakavyokifanyia kazi hicho kitu ulichokiamua basi hamu yote ya kufanyia kazi hicho ulichoamua huwa inapungua na unaweza ukajikuta unaairisha.
Katika mafanikio kuna hatua sita za muhimu za kuzingatia leo nataka kuzungumzia KUAMUA tuu nyingine tutajadili siku nyingine.
Inawezekana umekuwa unaamua mara kwa mara kuhusiana na mambo kadhaa kwenye maisha yako labda unataka kubadili kipato chako huridhiki na kile unachokipata,au unataka kuimarisha uhusiano wako na familia yako, au unataka kuanzisha biashara fulani, au unataka kuongeza maarifa juu ya jambo fulani lakini ukajikuta ni mtu wa kuamua na kuairisha hivyo basi ukawa hupati matokeo yoyote kwenye maisha yako.
Kuairisha baada ya kuamua inamaanisha mlango bado umefungwa hata kama ulikuwa umeamua kitu kizuri kiasi gani,kuairisha inamaanisha kile ambacho kilikuwa kinatakiwa kufanywa hakifanywi au hakitaweza kutokea,kuairisha inamaanisha kwamba fursa fulani ambayo ungeweza kuipata hutoweza kuipata kwa maana nyingine kuairisha ni mwizi wa fursa.
Katika kitabu cha Think and Grow Rich kilichoandikwa na Napolion Hill amesema kwamba watu waliofanikiwa sana na kuweza kujikusanyia kiasi kukubwa cha fedha ni wale ambao walikuwa wanaweza kufanya maamuzi kwa haraka na kuyabadili taratibu endapo tuu iliwabidi kufanya ivo.
Henry Ford kwa sababu hiyo hiyo ya kubadili maamuzi taratibu pale inapobidi ndiyo ilimfanya aendelee kutengeneza gari baya kuliko yote ulimwenguni lililokuwa linaitwa model T wakati washauri wake wote walimshauri aache kulitengeneza. Kitu ambacho watu hawajui ni kwamba alijikusanyia fedha nyingi kwa uamuzi huu maana lilikuwa linauzwa fedha kidogo na lilinunulika mno.
Katika maisha yako wewe ukiwa ni mtu wa kuendeshwa na maoni ya kila mtu basi ujue hutokaa uweze kuwa na maamuzi yako binafisi. Kuna kipindi kinafika mtu inabidi ufanye maamuzi yako mwenyewe ukae utulie usikilize moyo wako unasema nini kisha ndipo ufanye kitu.
Na kitu ambacho wazazi wengi wanakosea ni kwamba huwa wanawafanyia maamuzi watoto wao katika kile wanachotaka kufanya kwenye maisha yao hakuna kitu kibaya kama hiki maana kama utamwambia mtoto wako awe daktari wakati ndani mwake anajiskia ni mwanasheria ni kwamba unakuwa unampeleka sehemu ambayo hataki na hatokaa apende kile anachokifanya.
Uamuzi wa kweli na ulio na mashiko ni ule ambao unatoka ndani ya mtu mwenyewe ndio anaoweza kuutendea kazi na akaleta mabadiliko katika jamii.
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema hivi kama nataka kuwa mimi natakiwa kuwa huru, sio mimi mke wangu anaefikiri natakiwa niwe, wala sio mimi watoto wangu wanafikiri natakiwa niwe,wala sio mimi rafiki na jirani wanaetakiwa niwe ila mimi naetaka kuwa mimi.
Fanya uamuzi leo wa kuwa wewe unaetaka kuwa wewe,,
TUTAENDELEA NA HATUA NYINGINE....
DARASA LA AFYA NA MAENDELEO BINAFSI LINAENDELEA NA KUMBUKA JUMATATU HII YA TAREHE 14/09/2015 LITAANZA RASMI JIANDIKISHE MAPEMA. NAMBA HII 0689 452 670 SEMA HELLO WWLF.
UNA SHIDA YEYOTE YA KUANDIKA RESEARCH PROPOSAL,BUSINESS PLAN , FUND PROPOSAL WASILIANA NASI PIA.
No comments: