MAGANOKO NGAKA AAHIDI MABADILIKO MAKUBWA IKIWA ATACHAGULIWA KUINGIA MADARAKANI.
Judith Ferdinand
Mgombea Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Maganoko Ngaka, amewaahidi wakazi wa kata hiyo, mabadiliko ya kimaendeleo, endapo atapatiwa ridhaa katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Aliyasema, hayo wiki hii kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za kumtambulisha na kumnadi mgombea Udiwani Wa Kata hiyo kupitia CCM, ulifanyika katika Uwanja wa Mji Mwema mtaa Wa Nyamanoro Mashariki wilayani humo.
Maganiko alisema, wananchi watakua hawajafanya makosa endapo watamchagua na kushinda katika uchaguzi huo, anajiamini uwezo wa kusimamia na kuyasemea matatizo yao nao.
Alisema, atahakikisha wakazi Wa Nyamanoro wanajengewa soko, kwa ajili ya wakina mama kufanyabiashara katika mazingira salama.
Pia alisema, atasimamia kata hiyo, inapata zahanati kwa ajili ya kurahisisha matibabu na kupunguza vifo vya mama na mtoto, ikizingatiwa jografia ya maeneo mengi ya kata hiyo ni mlima.
Alisema, atasimamia na kuhakisha kituo cha polisi kinajengwa, licha ya kuwa ni mpango wa miaka mingi lakini viongozi walio pita walishindwa kutekeleza.
Hata hivyo alisema, atahakikisha suala la ajira kwa vijana wanalipatia ufumbuzi, kwa kuwafundisha ujasiriamali na kuwawezesha kifedha kutoka kwa wadau mbalimbali.
Aidha alisema, mabadiliko ya kimaendeleo katika Kata hiyo, atayasimamia na kutekeleza ilani ya chama hicho kwa kushirikiana na wananchi, kwa suala la maji,miundo mbinu , elimu na michezo.
No comments: