LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKAMPUNI YA PAMBA YAILALAMIKIA CDTF.

Na:Shaban Njia
Kutokana na Mfuko wa Wakfu wa kuendeleza zao la Pamba hapa Nchini (CDTF) kutofikisha fedha za ruzuku kwa Makampuni ya ununuzi wa Pamba, kumesababisha baadhi ya Makampuni kuacha kununua zao hilo huku mengine yakifa kutokana na ukosefu wa fedha.

Akiongea na Gazeti hili Meneja wa Kiwanda cha uchambuaji wa pamba Cha NIDA kilichopo Mjini Kahama Akbar Mohamed, alisema kuwa makapuni mengi ya ununuzi wa Pamba yameacha kununua zao hilo huku mengine yakibadilisha biashara kutoka na kutopata fedha za Ruzuku za kulipia Pembejeo kwa wakulima pamoja na dawa.

Menja huyo aliendelea kusema kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha za Ruzuku za Makampuni ya ununuzi kupitia Mfuko wa Wakfu wa kuendeleza zao hilo hilo lakini fedha hizo zimekuwa hazifiki kwa Makampuni hayo na wakati mwingine hufika kwa kiwango cha chini.

“Tunaiomba Serikali yetu ijayo kama itaweza itufikishie fedha zetu za Ruzuku bila ya kutumia Mfuko huo kwani kama sisi Wanunuzi wa zao la Pamba katika Wilaya ya Kahama tuna umoja wetu wa Makapuni ya ununuzi ambao unaitwa UMWAPA ambao serikali inaweza kupitishia hizo”, Alisema Akbar Mohamed Meneja kiwanda cha NIDA.

Alisema kuwa katika kipindi cha nyuma kulikuwa na zaidi ya Makampuni 50 ambayo yalikuwa yakijishghulisha na ununuzi wa zao la Pamba katika kanda ya ziwa lakini baada ya kukosa Ruzuku yamebakia makampuni 15 ambayo hata hivyo yanaweza kupungua katika msimu ujao na kubaki nane.

Pia Meneja huyo wa NIDA hakusita kuiomba Serikali kujenga Benki ya Wakulima ambayo itakuwa ikiwakopesha kwa Riba ndogo hali ambayo inaweza kufufua zao hili kama ilivyokuwa katika kipindi cha nyuma na Wakulima kuweza kufaidika na kuinua uchumi katika  ngazi za familia.

Aidha Meneja huyo alisema kuwa kwa sasa Mabenki yanatoa jumla ya asilimia 18 mpaka 20 ya riba kwa makapuni hayo halia mbayo hadi kuifikia kuisha kwa Msimu wa Pamba kwa mwaka huu umoja huo wa Makampuni ya Ununuzi wa zao la Pamba UMWAPA wanadaiwa jumla ya shilingi milioni 800 kama riba karika kiasi cha shilinngi bilioni nne walizokopa kununulia Pamba mwaka huu.

Meneja huyo wa NIDA aliendelea kusema kuwa Kampuni yake ilitoa kiasi cha shilingi milioni 600 kwa Wakulima kwa kununua dawa pamoja na Pembejeo lakini hadi kufikia hivi sasa ni asilimia 20 ya fedha hizo ndizo zimeweza kurejeshwa hali ambayo itaitia hasara kubwa Kampuni yake kwa mwaka huu.

Umoja wa Makampuni ya ununuzi wa zao la Pamba (UMWAPA) Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ulikopoa kiasi cha zaidi ya bilioni nne kwa ajili ya kuwakopesha wakulima Dawa pamoja na Pembejeo Za kilimo huku ikigharamia mafunzo kwa baadhia ya Maafisa Ugani Vijijini kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa Pamba kwa mwaka huu lakini hali imeonekana kuwa tofauti kwa msimu huu kuwa na kiwango kidogo cha uzalishaji.

No comments:

Powered by Blogger.