LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHAHIMIZA KUBORESHWA KWA SOKO KUU LA MJINI KAHAMA.

Na:Shaban Njia
Chama cha Tanzania Aliance for  change Transparency (ACT Wwazalendo) Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kimeitaka Halmashauri ya mji wa kahama kuliboresha soko kuu kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali za ukosefu wa huduma muhimu kwa wafanyabiashara wake kama choo, mitaro ya kupitisha maji taka pamoja kukosa dampo la kuhifadhia taka.

Malalamiko hayo yalitolewa jana na mwenyekiti wa chama cha ACT wazalendo Wilayani Kahama Idsam Mapande wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko la wakulima huku lengo kuu likiwa ni uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa mbunge.

Aidha Mapande alisema wafanya biashara wa soko hilo wamekuwa wakikosa huduma za msingi za kibinadamu kutokana na soko hilo kukabiliwa na changamoto nyingi kama choo mitaro ya kupitisha maji machafu katika kipindi cha masika na sehemu ya kutupia uchafu na ukosefu wa maji hali inayoweza kutokea kwa magonjwa ya mlipuko na kipindupindu.

Aliongeza kuwa  kwa kipindi kirefu sasa halmashauri ya mji wa Kahama imeshindwa kutatua kero hizo na sasa inadaiwa kuwa Wilaya ya Kahama imepanda hadhi na kuwa halmashauri ya Manispaa huku suala la usafi limewashinda na kuongeza kuwa soko hilo lililobeba jina la mji mzima  likiwa halina hadhi ya kuwa soko la Manispaa kwa kukosa huduma za msingi.

Mwenyekiti huyo aliitaka serikali kubomoa chumba cha ofisi ya soko hilo badala yake kijengwe choo cha kisasa ili wafanyabiashara hao wapate huduma hiyo ya msingi kwa binaadamu kwa kuwa ofisi hiyo ipo kama pambo la soko hilo hali ambayo inaweza kupunguza kero hiyo.

“Nawaombeni sana wana Kahama msiwachague viongozi ambao wakirudi kwenye majimbo yao wanafikia katika nyumba za wageni chagueni viongozi wenye uzalendo na Wilaya yetu ya Kahama ambao watatuletea maendeleo kwa pamoja msirubunike na elimu yao pamoja na pesa zao”. Alisema Mapande.

Kwa upande wake mgombea Ubunge wa jimbo la Kahama mjini kwa tiketi ya chama cha ACT wazalendo Bobson Wambula alisema kuwa samabamba na hayo Mji wa Kahama bado unakabiliwa na changamoto nyingi za ukosefu wa miundo mbinu za barabara, maji, Afya pamoja na tatizo sugu la kukatika ovyo kwa umeme hali inayohitaji kiongozi mzalendo wa kutatua changamoto hizo.

Pia Wambula aliwataka wananchi wa mji huo kuchagua kiongozi mzalendo atakayeweza kushughurikia changamoto zilizopo mbele yao na siyo kuchagua kiongozi kwa kufuata ushabiki wa kisiasa kwani watambue kuwa uongozi uliopita ngazi ya Ubunge haukuwasaidia chochote kutokana na raslimali zilizopo katika Wilaya yao.

No comments:

Powered by Blogger.