HII NDIYO KAULI YA MHE.ASHA-ROSE MIGIRO KWA WANAWAKE NCHINI.
Na:George GB Pazzo
Waziri
wa Katiba na Sheria Asha Rose Migiro amewasihi Wanawake nchini Kushikamana kwa
pamoja katika kutetea Maslahi ya Taifa hususani katika kuombea amani iliyopo
katika kuelekea kwenye kipindi cha Uchaguzi Mkuu.
Migiro alitoa Kauli hiyo jana Jijini Mwanza
alipokuwa akizungumza katika Kongamano la Wanawake na Maendeleo, lililoandaliwa
na Asasi ya Nitetee Foundation kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza kwa lengo la kuombea amani ya Taifa pamoja na Uchaguzi Mkuu.
Alisema kuwa ajenda ya wanawake nchini ni amani
hivyo wanapaswa kushiriki ipasavyo katika kuienzi kwa vitendo amani hiyo ikiwa
ni pamoja na kushiriki katika utatuzi wa matatizo ya kijamii ikiwemo kukemea
ukatili katika jamii pamoja na kutetea maslahi ya wanawake.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mwajuma Nyiluka ametoa rai kwa wanawake kuhakikisha
kuwa Uchaguzi Mkuu nchini unafanyika kwa amani
kwa kuwa wanayo nafasi hiyo kupitia maombi yao.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Asasi ya Nitetee
Foundation ya Jijini Mwanza Flora Lauwo amewaomba wadau mbalimbali kushirikiana
na asasi hiyo ili kufanikisha malengo yake ambayo ni kutoa elimu juu ya masuala
mbalimbali ya kijamii ikiwemo ujasiriamali, ukatili wa kijinsia, Mauaji kwa watu
wenye ulemavu wa ngozi pamoja na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu nchini.
TAZAMA HAPA PICHA ZA KONGAMANO HILO
No comments: