LIVE STREAM ADS

Header Ads

MATATA AZINDUA KAMPENI ZAKE KWA KISHINDO. ASEMA HATAWAANGUSHA WAPIGA KURA WAKE.

Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kitangiri, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kimezindua rasmi Kampeni zake ambapo Mgombea Udiwani katika Kata hiyo Henry Mtinda Matata ambae ni diwani wa Kata hiyo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela anaemaliza muda wake amewaahidi wananchi wa Kata hiyo kuwa hatawaangusha kiutendaji ikiwa kama watamchagua kuwa diwa wao.
Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Viwanja vya Minazi Mitatu, Kona ya Bwiru na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Kitangiri pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Katibu Mwenezi wa chama hicho Wilayani Ilemela Mussa Magabe pamoja.
Na:George GB Pazzo
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kitangiri Wilayani Ilemela kwa tiketi ya CCM Henry Mtinda Matata akipongezwa na Wakazi wa Kata hiyo katika uzinduzi wa Kampeni zake uliofanyika jana katika viwanja vya Minazi Mitatu Kona ya Bwiru Ilemela.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kitangiri Wilayani Ilemela kwa tiketi ya CCM Henry Mtinda Matata akiwahutubia wakazi wa Kata hiyo ambapo aliomba ridhaa ya kuwa diwani wao ili aweze kusimamia utekeleza wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika kata hiyo.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kitangiri Wilayani Ilemela kwa tiketi ya CCM Henry Mtinda Matata alisema kuwa akipata ridhaa ya kuwa diwani wa Kata hiyo atahakikisha anamaliza kero ya maji katika maeneo ya milimani ikiwemo Mitaa Ibanda na Mwinuko pamoja na kufikisha nishati ya umeme katika mitaa hiyo ambapo shughuli hiyo tayari imeanza katika awamu yake ya kwanza ya uongozi wake.

Pia alisema atahakikisha anasimamia vyema ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika Kata hiyo pamoja na kuboresha zaidi huduma za afya, mikopo yenye riba nafuu kwa akina mama, vijana pamoja na kuboresha maslahi kwa wazee. 
Katibu wa CCM Wilayani Ilemela ambae pia ni Mgombea Udiwani Kata ya Igoma Jijini Mwanza Mussa Magabe alisema kuwa hatima ya Tanzania iko Mikononi mwa Chama cha Mapinduzi hivyo wananchi wasifanye makosa katika kuwachagua viongozi wao kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais wahakikishe kuwa wanawachagua viongozi wanaotokana na chama hicho.
Mgombea Ubunge Jimbo la Geita Mjini (CCM) John Constantine Kanyasi akisalimia katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kitangiri Jimboni Ilemela.
Wakati wa Kitangiri wakifuatilia  Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Kata hiyo uliofanyika jana katika Viwanja vya Minazi Mitatu Kona ya Bwiru.

No comments:

Powered by Blogger.