LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU JIMBO LA TARIME MJINI.

Chama cha Alliance For Change and Transparency ACT Wazalendo Jimbo la Tarime Mjini Mkoani Mara jana kilizindua Kampeni zake za Uchaguzi Mkuu katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Serengeti.
Katika Uzinduzi huo, Deogratius Meck ambae ni Mgombea Ubunge (Mwenye Kinasa sauti) aliwaomba wakazi wa jimbo hilo kuwachagua viongozi wanaotokana na chama hicho kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais kwa ajili ya mabadiliko ya kweli katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja utatuzi wa kero ya miundombinu ya barabara na Maji katika jimbo hilo.
Na:Binagi Media Group
Wakazi wa Jimbo la Tarime wakifuatilia Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu za Chama cha ACT Wazalendo katika Jimbo hilo uliofanyika jana
Deo Meck ambae ni Mgombea Ubunge katika Jimbo la Tarime akihutubia katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu za Chama cha ACT Wazalendo katika Jimbo hilo uliofanyika jana.
Kulia ni Mke wa Mgombea Ubunge katika Jimbo la Tarime Mjini kupitia ACT Wazalendo akiwaombea kura wagombea wa chama hicho katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni zake za Uchaguzi Mkuu katika Jimbo hilo uliofanyika jana
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo ambae pia ni Mgombea udiwani Kata ya Nyamisangura akiomba kura katika Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu za chama hicho Jimbo la Tarime Mjini.
Kulia ni Mgombea Udiwani Kata ya Sirari kupitia ACT Wazalendo
Kushoto ni Mgombea Udiwani Kata ya Nyamisangura na Kulia ni Mgombea Udiwani Kata ya Sirari wote Kupitia Chama cha ACT Wazalendo
Mwenye kinasa sauti ni Mmoja wa waliorudisha kadi ya Chadema na Kujiunga na ACT Wazalendo
ACT Wazalendo
ACT Wazalendo
ACT Wazalendo
Mkazi wa Jimbo la Tarime Mjini akionyesha Kitabu kilichoandikwa na Mgombea Ubunge kupitia ACT Wazalendo katika jimbo hilo juu ya aliekuwa mbunge wa Tarime kupitia Chadema Marehemu Chacha Zakayo Wangwe

BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII

No comments:

Powered by Blogger.