DK.SLAA ATANGAZA RASMI KUACHANA NA SIASA NDANI YA VYAMA VYA VYA SIASA.
Aliekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dk.Wilbroard Slaa akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam hii leo.
Na:Binagi Media GroupAliekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dk.Wilbroad Slaa hii leo ametangaza rasmi kuachana na siasa.
Slaa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam na kubainisha kuwa ameachana na siasa ndani ya vyama vya siasa japo anaweza kuwatumikia watanzania bila kuwa na chama cha siasa.
Slaa ametumia muda mwingi kumzungumzia Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Edward Lowasa ambae kwa sasa ni mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chini ya mwamvuli wa Muungano wa Katiba ya Wananchi Ukawa.
Ametoa shutuma nyingi juu ya Mh.Lowasa kuhusiana na sakata la Richmond ambapo amemtaka aeleza ukweli juu ya sakata hilo.
Slaa amesema hataweza kujiunga na chama chochote cha siasa japo ataendelea kuyasimamia yale anayoyaamini kwamba hataogopa chochote.
"Nina uchungu mkubwa pale ninapoona chadema niliyoijenga ambayo haikuwahi kujaza watu kwa mabasi katika mikutano yake ya siasa leo hii inajaza watu kwa mabasi, wote mlijionea pale jangwani". Amesema Slaa.
No comments: