OJADACT YAZIDI KULIA NA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI AMBAYO IMEANZA KUTUMIKA LEO.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uharifu nchini OJADACT Edwin Soko akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Chama hicho zilizopo Jijini Mwanza juu ya Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ilioanza kutumika Rasmi hii leo hapa nchini.
Picha na George GB Pazzo
Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari nchini.
Sheria ya makosa ya jinai ya kimtandao 2015…1/9/2015…Jengo la CCM
Mkoa wa Mwanza.
Ndugu waandishi wa
habari tumewaita hapa
kwa ajili ya kuongea
nanyi juu ya
kuanza rasmi hii leo
kutumika kwa sheria ya
makosa ya kimtandao na ile
ya miamala ya
kielektoniki.
Sheria ya
makosa ya mtandaoni kwa ujumla
inaainisha makosa yanayohusiana
na matumizi ya mfumo wa kompyuta na
teknolojia ya habari na mawasiliano, na kuweka utaratibu
wa upelelezi, ukusanyajina matumizi
ya ushahidi wa kieletroniki.
OJADACT kwanza
tunaipongeza serikali kuleta
sheria hii ili kuendana na
kasi ya
kukua kwa teknolojia na kuongezeka
kwa vitendo vya
kihalifu Tanzania.
UCHAMBUZI WETU JUU YA SHERIA HII Uzuri wa sheria hii.
(1)Sheria hii bado ina tija kubwa ya
kuthibiti vitendo vya uhalifu wa kimtandao kama kutuma picha za ngono, wizi wa fedha,
kuandika uchochezi,kuandika
matuzi na kuzusha taarifa za uongo, kusababisha ajali na nyinginenzo.
(2)Sheria hii ina nafasi kubwa katika kulinda maadili ya taifa, hasa kwa kutoruhusu sasa matusi, uongo na uzushi kuwekwa mtandaoni.
Changamoto za sheria
hii
(1)Sheria hii itafanya Nchi kuwa adui wa
matumizi ya mtandao na teknolojia ya habari na mawasiliano kutokana na muundo wa sheria husika.
(2)Sheria inaminya uhuru wa mawasiliano mtandaoni ilivyobainishwa kwenye sheria mama ya Nchi ambayo ni katiba,
kwani hata jambo
ambalo ni la kweli lakini
likitafsiriwa ni uzushi au uongo basi mtoa taarifa atashughulikiwa na hivyo itapelekea watu wengi kuogopa kutoa taarifa yoyote ile.
(3)Sheria hii itahitaji zaidi mchango wa kimahakama katika kuamua kipi ni kosa na kipi sio kosa kwa mujibu wa sheria
kati ya mtoa taarifa na mpokeaji taarifa na mazingira ya
taarifa hiyo.
(4)Sheria pia inahitaji mchango mkubwa wa kitafsiri kwani neno matusi yanaweza kuwa na mgongano mkubwa na maana ya kimaudhui, ambayo yanaweza
pia kuonekana sio matusi.
Mambo ya kuepuka ili kuwa salama na sheria hii
·Epuka kusambaza ujumbe wa uchochezi
ama ushawishi
·Epuka kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi
·Epuka kusambaza picha chafu/utupu
·Epuka wizi wa kupitia mitandao
·Epuka kushiriki kumchafua mtu
·Epuka kupoteza simu bila kutoa taarifa
·Epuka kumpatia mtu lini yako ya simu
Ndugu waandishi wa habari tunawaomba sana kuwa makini na sheria hii na pia kuihabarisha jamii kuwa makini pia na sheria hii kwa lengo la kutoishia gerezani au kulipa au vyote kwa pamoja.
Imetolewa na;
Edwin Soko
Mwenyekiti Ojadact
Mwenyekiti wa Ojadact Edwin Soko
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uharifu Nchini OJADACT Edwin Soko akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Chama hicho zilizopo Jijini Mwanza juu ya Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ilioanza kutumika Rasmi hii leo hapa nchini.
No comments: