LIVE STREAM ADS

Header Ads

KITUO CHA POLISI NYANG’WALE MKOANI GEITA CHAPIGWA JEKI NA KAMPUNI YA ACACIA.

Na:Shaban Njia
Kampuni ya Acacia Bulyanhulu kupitia kitengo chake cha utafiti wa Madini imetoa Msaada wa vifaa mbalimbali vya Ofisi vyenye thamani ya shilingi milioni 18 kwa Kituo cha Polisi cha Karumwa Wilayani Nyang’wale Mkoani Geita kwa lengo la kuendelea kukuza mahusiano baina ya pande hizo mbili.

Akikabidhi Msaada huo kwa katibu Twala wa Wilaya ya Nyang’wale aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Biteyamanga Masudi, Mkuu wa Ulinzi wa Kampuni ya Acacia Tanzania John Bwana alisema kuwa Kampuni yake imeona vema kusadia kituo hicho kama moja na misaaad inayotolewa kwa maeneo yaliyo jirani na Mgodi kwa lengo la kukuza mahusiano.

Bwana alisema kuwa kutokan na Wilaya hiyo kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi kwa nguvu za Wananchi na Serikali ikaona ni vema kutoa msaada huo wa thamani za kituo ikiwa ni kukamilisha ombi lilitolewa na uongozi wa kituyo hicho kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Michel Ash siku za nyuma.

Mkuu huyo wa Ulinzi wa Kampuni ya Acacia Tanzania alivitaja baadhi ya vitu vilivyotolewa na Mgodi kuwa ni pamoja na Meza tano kwa ajili ya kopyuta, Viti 19 vya kisasa kwa ajili ya matumizi ya ofisi,  pamoja na makabati kwa ajili ya kuhifadhi nyaraka mbalimbali za kiofisi katika Jeshi hilo la Polisi.

Akitoa Shukrani kwa niaba ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Nyang’wale Sajent G 8086 D/C Jikolo alisema kuwa jeshi hilo la Polisi limefarika baada ya kupata msaada huo wa thamani za ofisi ingawa bado kuna changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi hilo kama vile ukosefu wa kopyuta za kufanyia kazi.

“Tunaomba angalau mtuangalie kwa upande wa pili ingawa mmetusadia thamani za kiofisi bado tunachangamoto kubwa kama vile ukosefu wa kompyuta kwa ajili ya kufanyia kazi kama tatu tukipata hizo moja tutaweka katika ofisi ya Mkuu wa kituo, nyingine kwa Mkuu wa Polisi na nyingine kwa Ofisa upelelezi wa Wilaya”, Alisema Jikolo.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyang’wale Biteyamanga Masudi alisema wao kama Wilaya wataendelea kukuza mahusiano na Mgodi wa Acacia Bulyanhulu ikiwa ni kama Wadau wakubwa katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika Wilaya hiyo.

Alisema kuwa awali Jeshi hilo lilikuwa na chumba kimoja ambacho kiliweza kutumiwa na Askari wote hali ambayo ilikuwa ni vigumu hata kuweka thamani katika ofisi hiyo kutoka na ilivyokuwa haikidhi hali ya utendaji wa kazi kwa Askari walikuwepo katika Wilaya hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.