WATUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI WATAHADHARISHWA.
Na:George GB Pazzo
Chama
cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu
nchini Ojadact kimewatahadharisha watumiaji wa Mitandao ya Kijamii kujihadhari
na Matumizi ya Mitandao yasiyo sahihi ili kuepuka kukumbwa na sheria ya makosa
ya mtandaoni ya mwaka 2015.
Tahadhari hiyo ilitolewa jana Jijini Mwanza na Mwenyekiti wa Chama
hicho Edwin Soko alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya sheria
hiyo ambayo imeanza kutumika rasmi hiyo jana.
Soko amewahimiza watumiaji wa Mitandao mbalimbali ya kijamii
kujiepusha na suala la usambazaji wa picha za utupu, matusi pamoja na ujumbe wenye
viashiria vya uchochezi kwa kuwa hayo ni miongoni mwa mambo yanayokinzana na
sheria hiyo.
Miongoni mwa adhabu anazoweza kukabiliana nayo mtumiaji wa mitandao ya
kijamii anaekiuka sheria hiyo ya Makosa ya Mitandaoni ya mwaka 2015 ni pamoja
na kufungwa gerezani katika kifungo cha hadi miaka 10 ama kulipa faini ambayo
inafikia hadi shilingi Milioni 30.
Wakati sheria hiyo inaanza kufanya kazi hii leo, baadhi ya watumiaji
wa mitandao mbalimbali ya Kijamii ikiwemo Blog, facebook na whatsupp wameeleza
kuwa ujio wake unaweza kukandamiza uhuru wa Watanzania kutoa na kupata taarifa
kwa njia ya mitandao huku wengine wakisema kuwa itasaidia kuimarisha matumizi
sahihi ya Mitandao hiyo.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
No comments: