LIVE STREAM ADS

Header Ads

HOTUBA YA DKT. SLAA YATIBUA MAMBO. VIJANA WA UKAWA JIJINI MWANZA WAJIUNGA NA CCM.

Vijana wa Ukawa waliokusanyika hii leo Jijini Mwanza kuunga mkono hotuba ya Dkt.Slaa aliyoitoa jana akitangaza kuanchana na siasa. Vijana hao wametangaza kujiunga na CCM.
 Na:Binagi Media Group
Siku moja baada ya aliekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dkt.Wilbroad Slaa kutangaza kuachana na Siasa, Vijana kutoka Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa Jijini Mwanza wameandamana na kutangaza kuachana na Vyama vyao na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.

Wakizungumza hii leo katika Viwanja vya Ghandh Hall Jijini Mwanza walipokuwa wamekusanyika,  Vijana hao wamesema kuwa wameamua kujiunga na CCM ili kuungana na Dkt.Slaa kupinga maamuzi yaliyochukuliwa na Viongozi wa Chadema katika kumsimamisha mgombea Urais ambae awali alikuwa akituhumiwa na kashfa za ufisadi.

Vijana hao Wameongeza kuwa hawako tayari kutumika kisiasa baada ya kubaini kwamba maamuzi yaliyochukuliwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe pamoja na Vyama vya Ukawa ya kumsimamisha Edward Lowasa kuwa Mgombea Urais hayakuwa sahihi na kwamba hatua inaashiria kuwa viongozi hao walinunuliwa.

Jana Dkt.Wilbroad Slaa alitangaza mbele ya Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam kuachana na Siasa baada ya kutokubaliana na maamuzi ya Viongozi wenzake ya Kumteua Edward Lowasa Kuwa Mgombea Urais wa Chadema kupitia Ukawa.
Vijana wa Ukawa waliokusanyika hii leo Jijini Mwanza kuunga mkono hotuba ya Dkt.Slaa aliyoitoa jana akitangaza kuanchana na siasa. Vijana hao wametangaza kujiunga na CCM.
Vijana wa Ukawa waliokusanyika hii leo Jijini Mwanza kuunga mkono hotuba ya Dkt.Slaa aliyoitoa jana akitangaza kuanchana na siasa. Vijana hao wametangaza kujiunga na CCM.
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii

No comments:

Powered by Blogger.