LIVE STREAM ADS

Header Ads

INASIKITISHA. MTOTO ASHAMBULIWA NA MBWA 20 NA KUPOTEZA MAISHA PAPO HAPO.

Mwili wa Mtoto Jovina (7) Mkazi wa Malimbe Jijini Mwanza baada ya umauti kumkuta kutokana na kushambuliwa na mbwa zaidi ya 20 (Tumeuziba ili kuzingatia maadili)
Picha na Linus
Ni Tukio ambalo limeacha simanzi na masikitiko makubwa kwa ndugu, jamaa na marafiki wa mtoto mmoja aliefahamika kwa jina moja la Jovina (7) Mkazi wa Malimbe Jijini Mwanza, baada ya kushambuliwa na mbwa wapatao 20 na kupoteza maisha papo hapo.

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tano asubuhi wakati mtoto huo alipokuwa ametumwa dukani na dada wa kazi (house girl) kununua mafuta ya kupikia.

Inaelezwa kuwa mbwa hao wanamilikiwa na wakazi wa eneo hilo na wamekuwa wakizagaa ovyo kutokana na kukosa matunzo bora.

Baada ya tukio hilo, wananchi walianza kuwasaka mbwa hao na kubahatika kuwaua baadhi yao lakini jambo la kusikitisha aliibuka mmoja wa wamiliki wa mbwa hao na kuanza kulaumu juu ya maamuzi ya wananchi hao hatua iliibua mtafaruku mkubwa.

No comments:

Powered by Blogger.