KAMPUNI YA ACACIA KUPITIA MGODI WA BUSWAGI ULIOPO MKOANI SHINYANGA YAIPONGEZA SERIKALI.
Na:Shaban Njia
Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi wa Buzwagi Mkoani Shinyanga imesifu juhudi zinazofanywa Serikali katika kuwajengea mazingira mazuri ya Utendaji kazi hali iliyofanya kampuni hiyo kuendesha shughuli zake kwa ufanisi katika uzalishaji wa Madini ya Dhahabu.
Hayo yalisemwa juzi na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Filbert Rweyemamu katika sherehe ya Siku ya Familia iliyofanyika katika Mgodi huo ikiwa na lengo ka kufahamiana na kutengeneza mtandao mkubwa wa mawasiliano na Wadau wa Mgodi huo.
Rweyemamu alisema kuwa Kampuni ya Acacia lazima iwe karibu na Serikali kwa lengo la kutengeneza mahusiano mema pamoja na Majirani wanaozunguka Mgodi huo waliopo katika kata ya Mwendakulima.
Alisema kuwa kupitia katika uongozi wa Kata ya Mwendakulima Mgodi umeweza kupata faida kubwa ya kuwashirikisha Wananchi hasa katika Shughuli za ulinzi na hivyo kuona Mgodi huo ni kama mali yao hali ambao imefanya mambo kama ya wizi kutokuwepo kwa kiwango kikubwa.
“Sisi kama Kampuni ya Acacia tumekuwa na mahusiano mazuri pamoja na ushirikiano na Wanachi wa Mwendakulima hasa katika masuala ya ulinzi kwani tumekuwa tukipata Walinzi wa Jadi wakitusaidia kulinda mali yetu kwani sisi wenyewe tusingeweza, Alisema Rweyemamu.
Pia Meneja huyo alisema kuwa Serikali ina uwezo mkubwa na kupitia kwao wameweza kufanikisha kazi ya kuleta maji ya Ziwa Victoria kutoka katika Mji wa Kahama hadi katika Mgodi huo na kuongeza kuwa Kampuni yake inalipa kiasi cha shilingi milioni 70 kama bili ya maji kwa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Kahama.
Kwa upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyekuwa Mgeni Rasmi katika sherehe hizo alisema kuwa yeye kama Srikali ya Wilaya ya Kahama anaomba soko la Madini ya Dhahabu lisiweze kushuka ili wawekezaji hao waendelee kubaki na kusadia wananchi wa Wilaya ya Kahama.
Alisema kuwa anajua kama Soko la Madini ya Dhahabu kwa sasa limeshuka lakini bado wanaomba wawekezaji hao wasibweteke kwani wao wamekuwa msaada mkubwa kwa Wananchi wa wilaya ya Kahama katika Nyanja mbalimbali kama vile Elimu, Afya, pamoja Maji.
Katika sherehe hjzo pia Kampuni hiyo ya Madini ya Acacia iliweza kuwatunukia baadhi ya Wafanyakazi wake bora ambao wameitumikia Kampuni hiyo kwa muda wa kuanzia miaka mitano hadi 15 zawadi za ufanyakazi bora uliotukuka.
No comments: