LIVE STREAM ADS

Header Ads

TEAM ESTHER MATIKO YAWASHUKURU WAKAZI WA JIMBO LA TARIME MJINI KWA MAPOKEZI YAO.

Msafara wa Esther Matiko (Pichani) ambae ni Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA chini ya Muungano wa Katiba ya Wananchi UKAWA ukitokea katika Kata ya Bomani ambapo mgombea huyo pamoja na wagombea wengine wa Udiwani kupitia ukawa walikuwa na Mkutano wa hadhara jana.
Na:Peter Magwi Michael,Team Matiko
"Kwa kipekee kabisa napenda kuwashukuru wale wote waliowezesha kufanikiwa kwa mkutano wetu wa jana Kata ya Bomani ndani ya viwanja vya shule ya msingi Buhemba.

Kwa niaba ya Team Matiko tumetambua jana uwepo wa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu aliefanya nasi campaign hiyo jana pamoja na viongozi wa chama wilaya.

Hakika jana ulikua ni mwendelezo wa juzi baada ya mkutano wa Nyamisangura, Umati wa watu wengi, wanachama na wapenzi walimsindikiza mgombea wetu kwa shangwe na furaha kutoka viwanja vya buhemba mpaka Ofisi za chama Wilaya.

Wale mlioko mbali bado tunawakaribisha Tarime kuendeleza mapambano mpaka tunatangaza ushindi kwa Kamanda wetu Esther Nicolaus Matiko."
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Tarime Lucas Ngoto akiwa ameongoza Msafara wa Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini kupitia chama hicho Esther Matiko
Umati wa wakazi wa Kata ya Bomani Jimboni Tarime wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za wagombea wa Ukawa uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Buhemba jana. 
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Visiwani Salum Mwalimu
Umati wa wakazi wa Kata ya Bomani Jimboni Tarime wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za wagombea wa Ukawa uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Buhemba jana. 
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Visiwani Salum Mwalimu
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini Chadema chini ya UKAWA Esther Matiko akiwahutubia wakazi wa Kata ya Bomani jimboni humo jana
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini Chadema chini ya UKAWA Esther Matiko akiwahutubia wakazi wa Kata ya Bomani jimboni humo jana
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Visiwani Salum Mwalimu akiwaombea kura wagombea wa Ukawa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika uwanja wa Shule ya Msingi Buhemba, Kata ya Bomani Jimboni Tarime Mjini.
Mabadilikoooooooo!!!!!!!
Esther Matiko (Kulia) akiteta jambo na Salumu Mwalimu (Kushoto) ambae ni Naibu Katibu Mkuu Chadema Tanzania Visiwani 
Salumu Mwalimu (Kushoto) ambae ni Naibu Katibu Mkuu Chadema Tanzania Visiwani akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Tarime Lucas Ngoto. 

No comments:

Powered by Blogger.