KAMPUNI YA ALAF YAWASIHI WATANZANIA KUNUNUA BIDHAA KULINGANA NA UBORA BADALA YA BEI NAFUU.
Mhandisi wa Kampuni ya Mabati ya ALAF(kulia) Daud Kidyamali akiwaelekeza wateja kuhusu ubora wa mabati hayo.
Picha na Judith Ferdinand
Judith Ferdinand na Sheila Katikula
Watanzania wameshauriwa kuangalia ubora wa bidhaa sokoni badala ya kuangalia zaidi gharama zake ili kueoukana na kuuziwa bidhaa zisizo na ubora.
Hii ni kutokana na watanzania wengi kukimbilia kununua bidhaa zenye gharama nafuu bila kuangalia ubora, hali inayopelekea kutumia kwa muda mfupi.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Afisa Mauzo wa Kampuni ya Mabati ya ALAF, Glory Kimaro wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Kampuni hiyo katika Maonyesho ya 10 ya biashara Afrika Mashariki, yanayofanyika katika uwanja wa chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology tawi la Mwanza wilayani Ilemela.
“Watanzania wanatakiwa kununua bidhaa kwa kuangalia ubora wa wakati ujao na siyo gharama kwa kipindi hicho, kwa kutokufanya hivyo watakuwa wanaua uchumi wa nchi kwa kushindwa kufanya vitu vya maendeleo na badala yake ni kurudia jambo moja kila mwaka". Alisema Kimaro.
Kwa upande wake Mhandisi wa Kampuni hiyo Daud Kidyamali alisema kuwa jamii inatakiwa kufanya tathimini ya bidhaa wanayoenda kununua bila ya kujali itagarimu kiasi gani.
Aliongeza kuwa jamii inatakiwa kufanya utafiti wa kuzungukia, kulinganisha na kukagua bidhaa zinazotengezwa na viwanda mbalimbali kabla ya kuzinunua ili kujua ni bidhaa ipi yenye ubora zaidi.
No comments: