LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA WASHAURIWA KUTUMIA VYUMA KATIKA UEZEKAJI WA NYUMBA BADALA YA MBAO.

Mhandisi wa kampuni ya ALAF(kulia) Daud Kidyamali akiwaelekeza wateja kuhusu ubora wa mabati hayo.
Picha na Judith Ferdinand
Judith Ferdinand na Sheila Katikula
Wakazi Mkoani Mwanza wameshauriwa kutumia vyuma kuezekea nyumba zao badala ya kutumia mbao jambo litakalosaidia katika utunzaji wa Mazingira na hivyo kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Wito huo ulitolewa juzi na Mhandisi wa Kampuni ya Mabati ya ALAF Daud Kidyamali, wakati akizungumza na BMG katika Monyesho ya 10 ya biashaya ya Kimataifa Afrika Mashariki katika uwanja wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology tawi la Mwanza wilayani Ilemela.

Kidyamali alisema kuwa ujenzi unaotumia paa za chuma unasaidia kutunza mazingira pamoja na kupambana na ukataji ovyo wa miti kwa ajili ya mbao.

"Kutokana na hatua hiyo tutapata hewa safi, mazingira yatakuwa bora, itazuia mmomonyoko wa udongo tutapata mvua za kutosha". Alisema Kidyamali.

Pia alibainisha kuwa uezekaji wa vyuma huondoa athari zitokanazo na wadudu waharibifu kama mchwa katika paa la nyumba, uimara na usalama wa nyumba katika kukabiliana na matetemeko ya ardhi pamoja na upepo mkali.

No comments:

Powered by Blogger.