LIVE STREAM ADS

Header Ads

MGOMBEA UDIWANI KATA YA TURWA WILAYANI TARIME AJA NA MFUMO TOFAUTI WA KAMPENI.

Nchini kote, Kampeni za Uchaguzi Mkuu zimepamba moto na Wagombea wanazunguka kila kona kukutana na Wananchi ili kuomba ridhaa ya kupigiwa kura na kuchaguliwa kushika nyadhifa wanazowania katika uchaguzi huo ambazo ni Udiwani, Ubunge na Urais.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Katika Kata ya Turwa, Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Mgombea Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Maendeleo CHADEMA  chini ya mwamvuli wa UKAWA Zakayo Chacha Wangwe (Wa tatu kushoto) ameamua kupita nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kuomba kura kwa wakazi wa Kata hiyo.

Itakumbukwa kuwa Zakayo Chacha Wangwe ni kijana wa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mwaka 2005 Chacha Zakayo Wangwe (CHADEMA) aliefariki dunia kwa ajali ya gari Julai 28,2008 akiwa Mkoani Dodoma akielekea Jijini Dar es salaam.

Wa pili kulia ni Mgomea Udiwani Viti Maalumu (Chadema) Kata ya Turwa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Mestica Steven na wa kwanza kushoto ni Katibu wa Chadema katika Kata hiyo Issaya Makoba.

No comments:

Powered by Blogger.