LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKALA: SERIKALI IZIKUMBUKE SHULE ZA SEKONDARI ZA BINAFSI NCHINI.

Wanafunzi wa shule ya sekondari mwalimu Tutuba iliyopo wilayani kibondo Mkoani Kigoma wakiwa katika chumba cha maabara katika shule hiyo,wakiwa katika mazoezi ya vitendo katika masomo ya sayansi.
Picha na Shaban Njia.
Na:Shaban Njia
Katika jambo lolote lile linalohitaji maendeleo ni budi jamii husika kuwa na mshikamano bila ya kujali jinsi na hali ya kipato kwa kushikamana ili kufanikisha hitaji linalokusudiwa.

Jamii inatakiwa kujitoa kwanza na kuonyesha ushirikiano hali ambayo inaweza kuleta mabadiliko chanya yatakayoweza kuwa mfano katika jitihada za kuibua kile ambacho hakikutarajiwa kufanyika.

Na katika kuhakikisha kuwa lengo linafanikiwa ni budi kwa Serikali kuona umuhimu wa kuweka mkono wake pasipo kujali kuwa jitihada hizo zipo kibiashara kwa kuwanufaisha Wamiliki hasa kwa kuwa manufaa yake yatakuwa na Tija kwa jamii nzima iliyopo.

Kutokana na hali hiyo kuna maeneo ambayo jamii na Wadau wamejitoa katika kuhakikisha kuwa mambo mbalimbali yanafanyika ili kuleta mabadiliko katika jamii lakini jitihada hizo zimekuwa zikikosa usadizi kutoka Serikali hali ambayo inakuwa ikiwakatisha tamaa.

Nchi ya Tanzania ilipata uhuru wake mwaka 1961 huku ikitangaza kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, Umasikini pamoja na maradhi lakini jitihada hizo zimekuwa kikwazo kutoka na Elimu kutoifikia jamii nzima hasa zile za pembezoni (Vijijini).

Pia inaeleweka kuwa msingi wa kupambana na maadui hao ni kwa jamii kupata Elimu ambayo itawafumbua macho na Serikali kutambua kuzidiwa na Mahitaji mbalimbali ya kijamii ilifungua milango kwa sekta binafsi kusaidia katika mapambano ya kuondoa ujinga kwa kuruhusu kuwepo kwa shule binafsi.

Aidha kutoaka na hali hiyo baadhi ya Wadau mbalimbali wa Elimu waliona ni mhimu katika kuisaidia Serikali jukumu hilo ambalo lilionekana kuizidi Uwezo kutokana na ongezeko la watu waliokuwa wakihitaji huduma hiyo ya Msingi.

Baada ya kuanzishwa kwa shule za Sekondari za Binafsi zilionekana kufanya vizuri zaidi kuliko zile za Serikali ambazo kwa kiasi kikubwa ndizo zilizokuwa zikipewa kipaumbele katika kupata Ruzuku mbalimbali zilizozisaidia katika kuziendesha shule hizo.

Lakini Serikali kwa sasa inapaswa kutambua kuwa jukumu la kueneza Elimu kwa Vijana kwa limekuwa likibebwa na shule Binafsi na si Shule za Serikali kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma hali ambayo imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya Elimu hapa nchini.

Pamoja na mapinduzi hayo makubwa ya Kielimu Serikali kwa sasa inapaswa kuelewa inajukumu kubwa la kuzisaidia shule za binafsi ambazo zimekuwa zikifanya vizuri siku hadi siku lakini zimekuwa zikikosa Ruzuku ya kuziendesha hali ambayo wamiliki wake wamekuwa wakitegemea Karo za Wazazi pamoja na Wadau mablimbali wa Elimu.

Inafahamika wazi kuwa Serikali ina majukumu makubwa katika sekta ya Elimu hata hivyo inatakiwa kutoa kipaumbele katika maeneo ambayo yamekuwa nyuma kielimu ambayo jamii ya sehemu hiyo kupitia Wafanyabiashara mbalimbali wa maeneo hayo wameonyesha jnia ya kuzisadia Sekondari zlizopo katika maeneo hayo.

Baadhia ya maeneo hayo ambayo bado mwamko wa Elimu upo nyuma yanapaswa kupewa kipaumbele ni pamoja na Wilaya ya Kibondo iliyopo Mkoani Kigoma ambaya kwa kiasi kikubwa bado Wananchi wake hawajawa na Mwamko wa kupata Elimu hususani ile ya Sekondari hata kama wakifaulu kwenda Shule za Serikali.

Pamoja na Mwamko huo Mdogo Baadhi ya Wafanyabiashara katika Wilaya hiyo wamejitokeza kumiliki Shule za Sekondari ambazo zimekuwa zikifanya vyema katika Mitihani nbalimbali Mkoani Kigoma japokuwa zinakabiliwa na Changamoto kubwa za uendeshaji Taasisi hizo.

Kufuatia hali hiyo Wadau na Wamiliki wa Shule hizo binafsi za Sekondari Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wameiomba Serikali kutoa Ruzuku kwa shule hizo ili kuweza kuhimili grarama za uendeshaji na kukuza sekta ya Elimu hapa nchini.

Wakiongea na Mwandishi wa Makala hii aliyekuwepo Mjini Kibondo hivi karibuni, Wadau hao wamesema kuwa kama Serikali itaweza kutoa Ruzuku kwa shule zisizokuwa za Serikali, suala la kuboresha Elimu hapa nchini litakuwa ni rahisi kwani kutakuwa na ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

Mmoja wa Wamiliki wa Shule binafsi nchini Salehe Makunga ambaye ni mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Mwalimu Tutuba Wilayani Kibondo amesema kuwa kwa sasa baadhi ya shule za sekondari zinazomilikiwa na watu binafsi zimekuwa hazifanyi vizuri kutokana na wamiliki wake kutokuwa na mitaji mikubwa kwa ajili ya uendeshaji wa shule hizo.

Aidha Makunga anasema kuwa kumekuwa na matatizo mbalimbali ambayo yamekuwa yakizikabili shule hizo kama vile kutokuwa na maabara kwa ajili kusomea wanafunzi masomo ya Sayansi na pia upungufu wa majengo hali ambayo kama serikali ingekuwa inatoa Ruzuku kungekuwa ahueni katika kufanikisha ukamilishaji wa mapungufu hayo.

Aidha Mwalimu Makunga anaendelea kusema kuwa kutokana na changamoto zilizopo katika shule hizo hususani shule yake, shule yake imejiwekea malengo makubwa ya kuboresha majengo yake pamoja ukamilishwaji wa vyumba vya maara hadi kufikia mwaka 2020.

“Tunashindwa kuboresha baadhi ya majengo katika shule hii kutokana na fedha nyingi tunategemea kutoka kwa wazazi hali ambayo mpaka kufikia hivi sasa hatuna fedha kwani hata hao wazazzi wanategemea kupata fedha zinazotokana na shughuli za kilimo wanazofanya hali ambayo inakuwa ni vigumu kuendeleza shule”. Anasema Makunga.

Pia Mwalimu huyo hakusita kuwalaumu baadhi ya wazazi katika Wilaya ya Kibondo kwa kutokuwa mstari wa mbele katika kuwasomesha watoto wao hasa katika Elimu ya Sekondari hata Pindi wanapofauli darasa la saba hali ambayo inachangia kuwa na mrundikano wa watoto ambao hawajapata elimu ya sekondari kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wake Mwalimu wa Taaluma katika shule hiyo Amos  Kilagambalaye anasema kuwa pamoja na shule hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali kuzisahau shule binafsi na kujikita na shule za serikali lakini shule hiyi imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya kiwilaya hadi kimkoa kwa muda miaka miwili iliyopita.

Kilagambalaye amewapongeza Wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kwa kuwa wasikivu pamoja na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha masomo hali ambayo inawatia moyo hata Walimu na wazazi wanaopenda Elimu katika Wilaya hiyo.

“Tumekuwa pia tukifanya vizuri kutoka na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya shule hii pamoja na  shule zingine zinazofanya vizuri hapa nchini kama vile St Marys ya Jijini Dare es Salaam hali ambayo inatuongerzea morari wa kuendelea kufanya vizuri siku za baadaye”. Anasema Mwalimu huyo wa Taaluma wa shule ya sekondari Mwalimu Tutuba.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya mwalimu tutuba wilayani kibondo Mkoani kigoma wakiwa mstarini(paredi) wakimsikiliza mwalimu wa zamu Amosi Kalambalaye hayupo pichana akitoa nasaha za masomo kabla ya kuingia darasani.
Picha na shaban Njia.

No comments:

Powered by Blogger.