LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUTANO WA LOWASSSA KAHAMA NUSURA UVUNJIKE KAHAMA.

Na:Shaban Njia
Jana Mkutano wa Mgombea Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia (UKAWA) Edward Lowassa nusura uvunjike baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (CHADEMA) Sebastian Thobias (KOMAA) kusema kuwa Mgombea huyo atachelewa kwa muda wa saa tatu hadi kufika katika Mkutano huo.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Wananchi wa Mji wa Kahama kutangaziwa toka juzi kuwa Mgombea huyo angewasili majira ya asubuhi na kuhutubia Wananchi ratiba ambayo ilienda kinyume na ilivyotarajiwa kwa kuchelea kwa muda masaa saba hali iliyoashiria kutoelewana kwa Viongozi wa Chadema na wananchi waliohudhuria Mkutano huo.

Hali hiyo ilirejea baada ya kuona ndege (CHOPA) ikizunguka katika maeneombalimbali yaMji wa Kahama ikitokea Wilaya ya Shinyanga Vijijini alipokuwa akifanya kampeni zake kabla ya kuja katika Mji wa Kahama kuendelea na Kampeni hizo

Hata hivyo katika Mkutano wake huo uliodumu kwa Muda wa nusu saa Mgombea urahisi huyo alitoa ahadi mbalimbali kwa  wakazi wa Mji wa Kahama ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa Benki ya Wachimbaji Wadogo Wadogo pmaoja na Machinga kwa lengo la kuwafanya kuwa Marafiki zake katika masuala ya kuondoa Umasikini.

Alisema kwa Sasa Wachimbaji wadogowadogo wamekuwa wakihangaika katika kutafuta mitaji kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji lakini imekuwa ni vigumu kupata hali ambayo kwa kuanzisha Benki hiyo inaweza kuwasaidia katikakupata mitaji ya kuendeshea shughuli zao hivyo kujikwamua katika janga la umasikini.

Lowassa aliendelea kusema kuwa iwapo atapata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania pia atahakikisha kuwa Machinga,Bodaboda pia wanakuwa karibu na Serikali yao na kuongeza katika uongozi wake hata penda kuona mtamzania nakuwa masikini huku rasilimali zikiwepo hapa nchini.

Awali aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akimkaribisha Mgombea Urais huyo Edward Lowassa alisema  Mji wa Kahama unakabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu mibovu, uhaba wa upatikaji wa umeme wakudumu licha ya Serikali ya CCM kuhaidi kutoa umeme katika Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA Buzwagi kuja katika Mji wa Kahama.

Alisema kuwa anamatumiani kuwa iwapo Edward Lowasa atapata Ridhaa ya kuwaongozwa Watanzania moja ya jitihadi ni kuhakikisha Mji wa Kahama unapata umeme wa kudumukutoka katika Mgodi wa Buzwagi na kuweka barabara za lami kutoka Mkoa wa Tabora kuiptia katika Kata za Kilago, Chambo Mhongolo hadi Mkoa wa Mwanza.

Pia Mgeja alimwomba Lowassa kuweka barabara za lami kutoka katika Mji wa Kahama hadi Mkoa wa Geita na pia kuhakikisha kuwa Bandari ya Nchi kavu iliyokuwa katika mji wa Isaka na kuhamishiwa Mjini Shinyanga inarudi ilikukuza uchumi wa Mji wa Kahama kwani Wafanyabiashara kutoka nchi za jirani za Burundi,Rwanda na Kongo wamekuwa wakiitemea sana bandari hiyokatika kusafirisha mizigo yao.

No comments:

Powered by Blogger.