LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI WA ROCKEN HILL SCHOOL YA MKOANI SHINYANGA ATOA ANGALIZO KWA WANAFUNZI NCHINI.

Na:Shaban Njia
Wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hapa nchini wametakiwa kusoma kwa bidii katika Elimu ya juu huku wakiwa na ndoto za baadaye hali ambayo itaweza kuwasaidia pindi wanapoanza maisha ya kijitegemea pamoja na wazazi wao.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Shule ya Rocken Hill Alexander iliyopo Mkoani Shinyanga Kazimiri katika mahafali ya 11 ya shule hiyo tangu kuanza kuhitimu kwa Elimu ya msingi katika shule hiyo na kuongeza kuwa kusoma bila ya kuwa na ndoto za baadaye  haisaidii chochote katika maisha .

Kazimiri alisema kuwa kazi ya kusoma ni pale unapokuwa na maono ya baadaye ya maisha ikiwa ni sambamba na kusimamia nidhamu unapokuwa shuleni na kusikiliza mafunzo kutoka kwa Walimu   hali ambayo inaweza kuleta mafanikio makubwa katika maisha.

“Ninawaambia Wanafunzi msome kwa bidii kama unataka kuwa Mwandisi lazima upende kusoma masomo ya Sayansi kama vile Phizikia, Bailogia pamoja na Kemia hali ambayo inaweza kukusaidia katika kufikia lengo la maisha yako ya baadaye”, Alisema Kazimiri.

Mkurugenzi huyo aliwataka Wazazi wa watoto wanaohitimu Elimu hiyo ya Msingi kujua kuwa Wanafunzi ndio bima yao ya uzeeni na kupitia kwao wanaweza kuona matunda yake pindi wanapofanya vizuri katika masomo yao hali ambayo wanaweza kuona mafanikio pindi wanapopata kazi nzuri na kuweza kuwasadia.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo yaliojumuisha jumla ya Wanafunzi 220 alisema kuwa
 Kwa sasa katika nchi ya Tanzania siasa zake zinahitaji usomi wa hali ya juu na kuongeza kuwa siasa za sasa sio kama zile za siku za nyuma.

Kamugisha alisema kuwa Siasa za sasa sio za kuvamia tuu kama ilivyokuwa hapo awali bali kwa sasa huna budi kusomea na kuongeza kuwa hata katika vyuo vikuu hapa nchini kwa sasa kuna watu wanaosomea Elimu ya Siasa hadi kupata Stashahada au Shahada kwa ajili ya Elimu hiyo hiyo.

Pia Kamanda Kamugisha alisisitiza masuala ya Ulinzi na amani nchini na kuwataka Watanzania kuacha kuwahifadhi Wageni wanakuja katika nchi yetu ambao hatuwajui kwani kwa sasa wema wa Watanzania umepita uwezo wa kuwakarimu hadi Wageni ambao hata hatuwajui wapotoka.

“Sisi tumekuwa tukiwahifadhi wageni kwa kiwango cha juu lakini kama na sisi tukienda katika nchi zao ukarimu huo haupo kwani wenzetu wamekuwa wakijenga hofu kubwa kwa wageni tofauti na ukarimu tunaowafanyia Watanzania wanapokuja hapa nchini”. Alisema Kamanda Kamugisha.

Hata hivyo Kamanda huyo alisisiza Wazazi kuwapeleka Watoto wao Shule ili kuepuka majanga yanayotokana na ukosefu wa Elimu kwani hata mauwaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanakuwa yakitokea mara kwa mara yamekuwa yakitokea kutoakana na watu kutokuwa na elimu na kuongeza kuwa kama watoto watasomeshwa na kuelimika hali itakoma.

No comments:

Powered by Blogger.