SEHEMU YA PILI: HATUA SITA MUHIMU MTU ANAZOTAKIWA KUPITIA ILI KUFANIKIWA.
Soma HAPA Sehemu ya Kwanza
HATUA YA PILI NI KUAMINI.
JE UNAAMINI HICHO UNACHOKITENDA KAMA NI SAHIHI.
Kuamini ni hisia ya kuwa na uhakika kwamba mtu fulani au kitu fulani kipo au kitu fulani ni cha kweli, hisia kwamba kitu fulani ni sahihi,kina thamani na ni kizuri.
Kwa mtu kuamini kitu kipo haimaanishi ni lazima awe amekiona Kwa macho yake anaweza kuamini kusikia au kusoma taarifa fulani, mfano wewe na mimi wote tunaamini kwamba kuna nchi ya China lakini inawezekana wewe hatujawahi kufika China kama mimi ukaiona lakini unaamini China ipo.
Baada ya kuamua nini unataka kufanya katika maisha yako kitu kingine cha msingi ni kuamini kwamba kile ulichoamua kinawezekana wewe kukipata. Wakati mwingine watu huwa wanaamua mambo ya kufanya katika maisha yao lakini hawaamini kwamba wanaweza kuyafanikisha.
Ni muhimu ukafahamu kwamba imani(faith) yako katika kutenda jambo fulani huwa huwa inaathiriwa na uwezo wako wa kuamini(belief).Kama kuamini kwako ni kudogo basi imani yako pia itakuwa ndogo vivyo hivyo.
Kwenye maisha yetu ya kila siku mtu hatakiwi kutamani/Kutakia(wish) kwamba maisha yawe mazuri maana hiyo haitoshi bali anatakiwa kuamini kabisa kwamba maisha yatakuwa mazuri na ya kupendeza kwa kufanya kile ambacho ameamua kukifanya katika maisha yake.
Kuamini kunajijenga katika maisha yetu kwa kufanyia tathimini yakinifu jambo/mambo mbalimbali, na pindi mtu anaporudia kufanya tena na tena tathimini kuhusiana na jambo fulani basi kuamini kwake katika lile jambo hubadilika moja kwa moja.
Ilikuwa inaaminika kwa wale waliosoma kitabu cha Things Fall Apart kwamba mama mjamzito hatakiwi kula mayai maana akila mtoto hatozaliwa na nywele baada ya watu kufanyia tathimini wakagundua sio kweli basi kuamini kwao juu ya hili kulibadilika moja kwa moja.
Mambo mengi ambayo leo hii tunayaamini na kuyaona kwamba ni sahihi na kweli nakuhakikishia mengi kati ya hayo hayapo sahihi kabisa na sio sisi tuliyaanzisha bali tuliyarithi kutoka kwa watu waliotutangulia na pindi utakapofanya tathimini yakinifu kwa nini ninaamini jambo fulani ndipo kuamini kwako kuhusu lile jambo kunabadilika.
Kuamini kunakuja kwa kujua na kufahamu uhusiano uliopo kati ya akili na mwili, jinsi vinavyofanya kazi kwa pamoja kwa kushirikiana, mwili ni mtenda kazi wa akili unafanya kile akili inachosema haijalishi kimetokea kwa mtu kukichagua kwa makusudi fulani(deliberatelly choosen) au moja kwa moja(automatically expressed)
Kitu ambacho kinatokea moja kwa moja (automatically expressed) ni kile kinachokuwa katika akili iliyolala(sub counsious mind) kama dhana fulani. Kama unataka kubadili maisha yako ni lazima ubadili hali(conditioning) katika akili yako iliyolala.
Watu wengi hawajui kwamba binadamu ana akili moja(mind) iliyogawanyika sehemu mbili ambazo ni counscious mind (akili iliyoamka) ni asilimia 10% na sub councious(akili iliyolala)asilimia 90%. Akili inayofanya kila kitu katika maisha yako ,mtendaji mkuu ni akili iliyolala. Akili inayoamua ni akili ambayo haijalala. Unataka kubadili maisha yako badili kile ulichokiweka katika akili iliyolala.
Jaribu kufanya zoezi hili hebu chukua peni na karatasi andika mambo ambayo unayaamini kwamba ni sahihi kwako baada ya hapo yafanyie tathimini(evaluation) hayo mambo katika kila jambo unaloliamini andika sababu tano za msingi kwa nini unaliamini kama ukikosa sababu tano basi jua huna sababu za kuamini hilo jambo achana nalo na tenda jambo lingine hii ndio namna ambayo wanasaikolojia waitumia kubadili mtu kutoka kuamini jambo fulani na kumuingizia jambo jingine.
#0689 452 670 WHATSUP US KWA MASOMO YA AUDIO NA NOTES PIA. DARASA LITAANZA TAREHE 14/09/2015 SAA 5:00 PM BURE WIKI YA KWANZA.
email allnhump@gmail.com
SHEA NA WENZAKO WENGI KADIRI UWEZAVYO, SIKU NJEMA,
LIKE OUR PAGE ON FACE BOOK LIFE SECRETS COMPANY!
No comments: