SIKU YA WAHANDISI NCHINI, WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA IMANI NA WAKANDARASI WAZALENDO.
Jengo la Kibiashara linalojengwa na Kampuni ya Kigeni Jijini Mwanza.
Na:George GB Pazzo
Watanzania
wameshauriwa kujenga imani na Wakandarasi wa ndani ya nchi na hivyo kutoa tenda za
ujenzi kwa Makampuni ya kizalendo badala ya kuwategemea wakandarasi kutoka nje
ya nchi.
Ushauri huo umetolewa hii leo Jijini Mwanza na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya JBM Civil Contractors Joseph Castus wakati
akizungumza na Radio Metro juu ya Siku ya Wahandisi nchini iliyoadhimishwa
Jijini Dar es salaam.
Castus amesema kuwa Serikali pamoja na Wananchi
wanapaswa kutambua kuwa wapo Wakandarasi bora nchini ambao wana uwezo wa
kujenga na kusimamia miradi mikubwa ya ujenzi hivyo tenda zinapotangazwa vipaumbele
zaidi vitolewe kwa Wakandarasi hao.
Pia meongeza kuwa Bodi za zabuni nchini bado
hazijawa na imani juu ya Wakandarasi wa ndani kutokana na Wakandarasi wengi
kukabiliwa na uhaba wa mitaji hatua ambao husababisha wakandarasi wa kigeni
kupewa miradi mingi ya ujenzi ambapo ameomba Serikali kuwawezesha Wakandarasi
hao kupitia Mikopo yenye riba nafuu.
Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini yameanza
hii leo na yanatarajia kufikia tamati kesho ambapo yamekuwa ni maadhimisho ya
13 tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2003 yakiwa yamelenga kuiwezesha jamii
kutambua michango tunu inayofanywa na wahandisi wa Tanzania katika maendeleo ya
kijamii na kiuchumi pamoja na kuwahamasisha vijana kusoma taaluma ya uhandisi.
No comments: