LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATISHIA KUTOPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU UNAOTARAJIA KUFANYIKA MWAKA HUUU.

Na:Shaban Njia
Wakazi wa kitongoji cha Sofi Kata ya Mhongolo wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametishia kutoshiriki katika zoezi la upigaji  kura katika uchaguzi mkuu octoba 25 mwaka huu, kutokana na kitongoji chao kutojengewa daraja linalounganisha kitongoji hicho na makao makuu ya kata.

Malalamiko hayo yalitolewa jana kwa vyombo vya Habari na wananchi hao kutokana na kilio chao cha muda mrefu cha ukosefu wa huduma za msingi,barabara,maji na umeme ambapo ni miaka mitatu sasa hawajatatuliwa matatizo yao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kitongoji hicho John Pumba alimlalamikia Diwani wa kata yao Daud Bandeke kwa tiketi ya CHADEMA kuwa ndiye aliyesababisha wananchi wa kitongoji hicho kususia kutoshiriki zoezi la upigaji kura kutokana kukisahau kijiji chao kuboresha huduma muhimu hususani miundo mbionu za barabara.

Pumba alisema kuwa kitongoji chao hugeuka kuwa kisiwa cha bahari katika kipindi cha masika ambapo malalamiko hayo walikuwa wakiyatoa marakwa mara kwa diwani wao na anayapuuza hivyo wamechoshwa na hali hiyo na kuona suluhisho muhimu ni kususia kupigia kura kwa chama chochote cha siasa kwani kipindi cha kujinadi huwapa maneno matamu.

“Mimi kama mkazi wa kitongoji hiki nasema kilio chetu kikubwa ni barabara inayounganisha kata na kitongoji hiki ili kwenda kupata huduma za msingi kutoka katika kitongoji chetu ambapo kipo umbali wa kilometa 25 hadi kufika makao makuu ya kata ya Mhongolo ambayo kimsingi tunapata shida wakati wa masika kwani serikali ingekuwa inafika huku ingetuhurumia tumekuwa kama sisi siyo watu wa Kahama”alisema Alphonce Longhwe mkazi wa kitongoji cha Sofi.

Hata hivyo mmoja wa kina mama ambao ndio wahanga wakubwa Seja Ramadhani alisema kuwa barabara hiyo kipindi cha masika hujaa maji kama bahari ya Hindi ambapo watoto wao kipindi chote cha masika hushindwa kufika shuleni kwaajili ya masomo, ambapo alisema kipindi hiki cha kampeni ili kuwapigia kura wanamuomba mgombea Uraisi kupitia CCM John Magufuli lazima afike kwanza katika kitongoji hicho ajionee mwenyewe.

Aidha Ramadhani alisisitiza kuwa wananchi watapiga kura kama mgombea huyo atafika katika kitongoji chao kujionea adha hiyo kubwa wanayoipata na kusema kuwa endapo magufuli hatafika katika kitongoji hicho hawatapiga kura zao ili kuchagua kiongozi kwani wamewadanganya vya kutosha.

“Safari hii bora tukae tu nyumbani tusijishughulishe na kuhangaika kuwapigia kura zetu watu wasio tuthamini katika maendeleo , tunasikia Halmashauri kupitia Baraza la Madiwani linatoa mafungu ya fedha za kukarabati barabara za kata pamoja na madaraja lakini sisi kitongoji chetu wakekisahau hasa kwa kipindi cha miaka mitano cha Diwani wetu Bandeke wa Chadema,leo hii tunyanyue miguu yetu tuwapigie tena hapana kabisa”alisema Ramadhani.

Akijibu tuhuma hizo Diwani aliyemaliza muda wake Daud Bandeke alisema kazi ya Diwani ni kukusanya kero zote na kuziwasilishwa Halmashauri,hivyo aliongeza kuwa hawana sababu ya kumlaumu kwani kazi aliyoifanya wana Mhongolo wanaifahamu na kusema hata hivyo kitongoji chao kipo kwenye ratiba lakini kinacho kwamisha ardhi yao inatitia hali inayoweza kusababisha Greda kuzama na kuongeza Diwani ajaye atamalizia.

“Mimi nilipoishia diwani mwenzangu ataendeleza na kama wanaona sijawatendea haki wamfuate Injinia wa Halmashauri kwani hata hivyo kazi ya diwani ni kukusanya kero zote za wananchi na kuwakabidhi Halmashauri ama mkurugenzi mimi nimemaliza muda wangu wambie wamfuate injinia kama barabara na daraja hawajatengenezewa”alisema Bandeke aliyekuwa Diwani.

No comments:

Powered by Blogger.