LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZAZI NCHINI WATAKIWA KUWARITHISHA ELIMU WATOTO WAO BADALA YA MALI.

Na:Shaban Njia
Wazazi nchini wametakiwa kuwahimiza watoto wao kuwa Elimu ndio msingi na urithi mkubwa katika maisha yao usiohamishika tofauti na kumrisisha Mwanafunzi mali ambazo zinaweza kuisha na kupotea kwa mara moja katika kipindi kifupi.

Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Anderleck Ridges ya Mjini Kahama Alexander Kazimiri katika mahafali ya saba ya kidato cha nne ya shule hiyo.

Kazimiri alisema kuwa kitendo cha wazazi kuwarisisha Watoto wao mali badala ya Elimu ni kuwapotosha kwani mali hizo zinaweza kupotea wakati wowote na kusababisha Umasikini mkubwa katika familia.

“Kwa sasa katika jamii suala la Elimu ni muhimu kwa watoto lakini Elimu hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwa ni sambamba na mmomonyoka mkubwa wa maadili unaochangiwa na mitandao inayotumiwa na watoto wetu”. Alisema Kazimiri.

Hata hivyo Kazimiri hakusita katika kulaani mauwaji ya watu wenye Ulemavu wa ngozi (Albino) na kuongeza kuwa mauwaji hayo yamekuwa yakifanyika kutokana na watu kukosa Elimu kwa kiasi kikubwa.


“Kwa sasa tunashuku mungu kuona hali hiyo ya mauwaji imeweza kupungua kwa kiasi kikubwa katika Mkoa wa Shinyanga na sasa hatuna budi kuendelea kutoa Elimu juu ya kukomesha kabisa hali hiyo na yasiweze kutokea tena katika siku za baadaye”. Aliongeza Kazimiri.

Takribani wanafunzi 164 wanatarajia kuhitimu masomo ya kidato cha nne katika shule hiyo ambapo wa idadi ya wanafunzi wa kike ni 42 hali ambayo bado inaleta changamoto kwa wazazi kuwapeleka shule watoto wa kike.

No comments:

Powered by Blogger.