BODABODA JIJINI MWANZA WATAKIWA KUWEKA SIASA KANDO.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Waendesha
pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda Mkoani Mwanza, wamehimizwa kuweka kando
itikadi zao za kisiasa na kujikita zaidi kwenye majukumu yao ya kazi badala ya
siasa kwa kuwa masuala ya uchaguzi mkuu tayari yamefikia tamati.
Rai hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa
Muungano wa Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda, wakati akizungumza
na Binagi Radio Habari ya Binagi Media Group.
Makoye alisema kuwa uchaguzi umekamilika hivyo
maisha yanapaswa kuendelea kwa kila mmoja kufanya kazi kwa bidii katika eneo
lake huku akisahau yale yote yaliyojitokeza katika mchakato mzima wa Uchaguzi
Mkuu.
“Tumemaliza Uchaguzi salama hivyo niwashukuru
waendesha pikipiki kwa hilo na kila mmoja aendelee kufanya kazi kwa bidii zaidi
kwani maisha ni kazi”. Amesema Kayanda.
Aidha alitoa rai kwa watumiaji wa barabara
wakiwemo bodaboda, kuzingatia suala la Usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuzingatia
utii wa sheria bila shuruti.
Katika harakati za Uchaguzi Mkuu mwaka huu,
waendesha pikipiki kote nchini walionekana kuwa na msukumo mkubwa wa kuambatana
na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi, pindi walipokuwa katika harakati
za kuomba kura kwa wananchi.
SIKILIZA RIPOTI KAMILI KUPITIA BINAGI RADIO
No comments: