LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHAWATAKA WAPINZANI KUKUBALI MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU.

Na:Shaban Njia,Kahama
Chama cha ACT Wazalendo Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kimesema kuwa ushindi alioupata Dkt.John Pombe Magufuli,Wabunge na Madiwani kupitia Chama cha Mapinduzi CCM katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka huu ulikuwa wa halali na wahaki.

Katibu Mwenezi wa Chama hicho Wilayani hapa Kasigwa Bwire alisema hayo majuzi katika sherehe za tathimini ya uchaguzi wa Madiwani, Urais pamoja Ubunge zilizojumuisha Wasimamizi wa Uchaguzi huo zilizofanyika kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama.

Kasigwa alisema kuwa katika uchaguzi huo hakuna mtu aliyeibiwa kura zake na kuongeza kuwa maneno yanayosemwa mitaani kuwa kulikuwa na uibwaji wa kura ni yauongo na wagombea wote waliopata ushindi walishinda kihalali.

Alivitaka vyama vilivyoshindwa katika uchaguzi kuonyesha ushirikiano na chama kilichopata ushindi na kuhakikisha kuwa hakuna ubaguzio wowote na kusimiamia kanuni, Sheria  za nchi na kuleta maendeleo kwa watanzania wote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa hafla hiyo Isabela Chilumba alisema kuwa lengo la kufanya hafla hiyo ni kufanya tathimini ya shughuli za uchaguzi ulimalizika kwa amani na upendo katika Wilaya ya Kahama.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa ambaye Alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alisema kuwa anawapongeza Viongozi wa madhehebu ya yote ya dini kwa kuwahimiza waumini wao juu umuhimu wa kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu kwa amani na utulivu..

No comments:

Powered by Blogger.