LIVE STREAM ADS

Header Ads

KITUO CHA MAKUZI YA WATOTO WADOGO KAMBARAGE JIJINI MWANZA CHAWANUSURU WATOTO KUKOSA ELIMU.

Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Hiki ni Kituo cha Makuzi ya Watoto Wadogo (Zaidi Miaka Miwili hadi Mitano) kilichopo Mtaa wa Kambarage Kata ya Igogo Jijini Mwanza kimekuwa mkombozi kwa watoto kupata elimu ya awali.

Ni kituo kilichoanzishwa na Serikali ya Mtaa huo kwa ajili ya malezi ya watoto (Day Care) ambapo mzazi/walezi huwaacha watoto wao katika kituo hicho asubuhi wakiwa wanaenda katika shughuli zao za kutwa na kuwafuata baada ya jioni.

Katika kituo hicho, elimu ya awali hutolewa kwa watoto hao hatua ambayo imesaidia watoto katika mtaa huo kupata elimu bora ya awali ambapo wazazi/walezi huchangia gharama kidogo ya shilingi 5,000 kwa mwezi hii ikiwa ni kwa kila mtoto.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Peter Kiberenge ameiambia BMG (Binagi Media Group) kuwa lengo la uongozi wa mtaa huo ni kupanua zaidi kituo hicho ili kiweze kutoa fursa ya kielimu kwa watoto wengi zaidi ambapo hadi sasa kituo kina watoto 80.
Kuna Michezo ya aina mbalimbali katika Kituo hiki cha Makuzi ya Watoto wadogo Kambarage, Kata ya Igogo Jijini Mwanza
Watoto wakifurahia michezo ya aina mbalimbali katika Kituo hiki cha Makuzi ya Watoto wadogo Kambarage, Kata ya Igogo Jijini Mwanza
Watoto wakifurahia michezo ya aina mbalimbali katika Kituo hiki cha Makuzi ya Watoto wadogo Kambarage, Kata ya Igogo Jijini Mwanza
Mpe Mtoto Malezi Bora
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kambarage, Kata ya Igogo Jijini Mwanza, Peter Kiberenge (Kulia) akiwa pamoja na Watoto walio katika Kituo cha Makuzi ya Watoto wadogo Kambarage.

No comments:

Powered by Blogger.