KLABU YA ROTARY YA DAR ES SALAAM OYSTERBAY WATOA MATIBABU YA BURE KWA WAKAZI WA KEREGE-BAGAMOYO.
Rais wa klabu ya Rotary Dar es Salaam Oyster Bay kwa mwaka huu wa 2015-2016, Mohamed Versi akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) katika mji wa Kerege jana Novemba 15. wakati wa zoezi hilo la kambi ya bure ya upimaji wa afya. (Picha zote na Andrew Chale ).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[BAGAMOYO] Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay, kwa mara nyingine tena imeendesha matibabu katika kambi maalum ya matibabu ya bure katika mji wa Kerege uliopo Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Kambi hiyo iliyofanyika siku ya Jumapil Novemba 15.2015 ambapo zaidi ya wahudumu 50 wa Afya walipima na kutibu magonjwa kwa wakazi hao wa Kerege waliojitokeza kwa wingi wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 700.
Kambi hiyo ya matibabu bure imedhaminiwa na benki ya Diamond Trust Bank (DTB) imeweza kuwa faraja kubwa kwa wananchi na wakazi wa Kerege kupata Huduma hiyo kwani imeweza kuwafikia muda muafaka kwao kupata fursa za matibabu na vipimo bure.
Akizungumza na wanahabari Rais wa klabu hiyo ya Rotary Dar es Salaam Oyster Bay kwa mwaka huu wa 2015-2016, Mohamed Versi amebainisha kuwa wito mkubwa kwa wananchi wa Kerege kujitokeza kunawapa faraja kuendelea kutembelea na kuweka kambi kwa mwaka mara moja katika mji huo.
“Mwaka huu ni wa tano tokea kuanza kutoa matibabu bure kwa kuweka kambi hizi za matibabu. Kwa hapa Kerege huu ni mwaka wa nne tunafika hapa na kuhudumia wananchi huku zaidi ya wananchi, 600 hadi 700 wanahudumiwa ikiwemo vipimo na matibabu” alisema Versi.
Aidha, Rais huyo alibainisha kuwa, mbali na kutoa matibabu bure pia wameweza kutoa dawa pamoja na neti za kuzuia mbu kwa kila mwananchi aalijitokeza kwenye kambi hiyo.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko kutoka benki hiyo ya DTB, Bw. Sylvester Bahati amebainisha kuwa kujitokeza kudhamini kambi hiyo ni miongoni mwa taratibu za benki hiyo kuweza kusaidia jamii.
“Tunawapongeza Rotary Klabu kwa kuona umuhimu wa kusaidia kambi hii ya Kerege matibabu bure na ufadhili wetu hapa unaendana na sawa na taratibu tulizojiwekea za kutoa gawio kwa jamii kama zilivyotaratibu nyingine tulizonazo” alibainisha Bw. Bahati.
Aidha, ameeleza kuwa Benki hiyo ya DTB ina matawi zaidi ya 20 nchini huku ikitarajia kufungua matawi zaidi kwa nchi nzima ikiwemo Zanzibar.
Kwa upande wake daktari na mratibu wa magonjwa ya Kisukari, Dk. Bashiru Rajab ameeleza kuwa, wengi wa wa wagonjwa walipatikana katika kambi hiyo ni wale wa matatizo ya mapigo ya moyo (Blood pressure ).
“Katika kambi hii wengi wa wananchi wanaofika hapa wanakabiriwa na matatizo ya Presha na ugonjwa wa Maralia huku wa kisukari wakiwa wachache. Inatia faraja sana kwani wamepata kujua hali ya afya zao za mwili na tunawashahuri wawe na taratibu ya kupima afya mara kwa mara” alibainisha Dk. Bashiru.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi walipongeza waandaaji wa kambi hiyo ambapo imewasaidia kujua afya zao hivyo kuchukua hatua ikiwemo suala la kuzingatia kanuni za kufuata pamoja na ushahuri wa kitabibu.
Matibabu, sehemu mojawapo ya Miradi ya Afya ya Jamii, ambayo hufanyika kila mwaka toka ilipozinduliwa mwaka 2011 katika kitongoji cha Chanika jijini Dar es Salaam ambapo takribani wananchi 600 walijitokeza kupima malaria, VVU, Kisukari, magonjwa ya mfumo wa upumuaji, macho na viashiria vya magonjwa sugu na baadae kuamia katika mji huo wa Kerege kwa mwaka wa nne sasa huku wakitoa dawa na miwani bure.
Kwa mwaka huu imedhaminiwa na benki ya Diamond Trust Bank, Rotary Club of Seattle4 huku ikiandaliwa kwa kushirikiana na Shree Hindu Mandal Hospital, Vital Supplies, Kids Care Tanzania, Elite Dantal Clinic, Whitedent, Sayona, Ultimate Security na wengine wengi.
Mkuu wa kitengo cha Masoko kutoka benki ya Diamond Trust Bank [DTB] akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa zoezi hilo la kambi ya matibabu bure. DTB ndio wadhamini wakuu katika kambi hiyo.
Daktari na mratibu wa magonjwa ya Kisukari, Dk. Bashiru Rajab akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo la kambi ya bure ya Matibabu katika mji wa Kerege,Bagamoyo Pwani.
Mkazi wa Kerege akiwa katika mstari wa kwenda kumuona Daktari kwa ajili ya kupima afya zake sambamba na mtoto wake wakati wa kambi hiyo Novemba 15.2015.
Zoezi la Kambi hiyo ya matibabu bure likiendelea katika mji huo wa Kerege..
Mmoja wa wananchi wa Kerege (kulia) akimwelezea Daktari wa kambi hiyo..
Upande wa huduma za macho...katika kambi hiyo
Kitengo cha dawa wakiwa tayari kwa kutoa huduma hiyo wakati wa kambi hiyo..
Wananchi wakipatiwa dawa bure wakati wa kambi hiyo..
Huduma ya kinywa ikiendelea..
Baadhi ya vifaa maalum kwa ajili ya matibabu ya kinywa ikiwemo meno kutoka Elite Dental Clinic wakati wa kambi hiyo..
Baadhi ya madaktari wa magonjwa ya kinywa wakiwa tayari kwa ajili ya kutoa huduma kwa mmoja wa wakazi wa Kerege aliyefika katika kambi hiyo. Huduma ya Kinywa ilitolewa na Elite Dental Clinic.
Huduma hizo za kinywa zikiendelea..
Picha za juu na chini ni eneo la upimaji wa magonjwa wa kinywa na meno iliyokuwa ikitolewa na Elite Dental Clinic
Mtaalamu wa tiba ya macho akiendelea na uchunguzi kwenye kambi hiyo
Zoezi hilo la upimaji likiendelea katika vitengo mbalimbali wakati wa kambi ya upimaji na matibabu bure katika mhi wa Kerege.
zoezi likiendelea kwa wananchi kupitia hatua moja hadi nyingine...
Baadhi ya wanachama wa Rotary Klabu ya Dar es Salaam Oyster Bay wakiwa katika kambi hiyo kutoa huduma..
Baadhi ya wananchi wa Kerege waliojitokeza wakiwa kwenye foleni katika Kambi hiyo huku wakipatiwa maelezo mbalimbali juu ya afya..
Baadhi ya wananchi upande wa wanawake waliojotokeza kwenye kambi hiyo..
Wananchi wakipata kusajiliwa kwa lengo la kuelekea kumuona Daktari na vipimo..
Baadhi ya waanachi hao wakiwa kwenye moja ya foleni kuingia kwa madaktari na vipimo mbalimbali wakati wa zoezi hilo.
Wananchi hao wakiwa katika kambi hiyo..
Huduma na somo likiendelea wakati wa kambi hiyo..
Soma zaidi hapa:
No comments: