LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAADHIMISHWE KWA VITENDO ZAIDI.

Na:Binagi Media Group
Tanzania leo inaungana na nchi nyingine duniani kuptia Mashirika ya Haki za Binadamu, Wadau wa Maendeleo na Asasi za Kiraia na wadau wengine wa haki za binadamu duniani kuanza maadhimisho ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Novemba hadi Desemba 10.

Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia ni tukio la kimataifa la kila mwaka linalolenga kujenga nguvu ya pamoja katika kuzuia vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia. Ndani ya siku hizi, kuna siku zingine muhimu za kimataifa ambapo Novemba 25 ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake, Novemba 29 ni Siku ya Kimataifa ya Watetezi wa Haki za Binadamu.

Desemba mosi ni Siku ya UKIMWI Duniani, Desemba 3 ni Siku ya Kimataifa ya watu wenye Ulemavu, Desemba 6 ni Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Mauaji ya kikatili ya Montreal ya mwaka 1989 ambapo wanawake 14 waliuawa na mtu (Mwanaume) aliyekuwa anawachukia wanawake. Desemba 10 ni siku ya Tamko Rasmi la La Haki za Binadamu.

Tarehe hizi zilichaguliwa mahususi ili kuunganisha Ukatili wa Kijinsia na Haki za Binadamu na kuweka msisitizo kuwa Ukatili wa Kijinsia ni ukiukwaji wa Haki za Binadamu na haukubaliki katika jamii.

Binagi Media Group inasisitiza kwamba, Maadhimisho ya mwaka huu wa 2015 ni vyema yakaadhimishwa kwa vitendo zaidi kuanzia ngazi ya jamii hadi ngazi za juu zikiwemo ngazi za Serikali pamoja na zile za mashirikika na taasisi binafsi ili kuhakikisha jamii vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii vinatokomezwa.

No comments:

Powered by Blogger.