LIVE STREAM ADS

Header Ads

MHANDISI MKUU JIJINI MWANZA AZUIA ULIPUAJI WA BARUTI UNAOFANYWA NA KAMPUNI YA LAKE HOLDING.

Mhandisi Mkuu wa Jiji la Mwanza Eng.Ezekiel Kunyaranyara amesimamisha kwa muda shughuli za upasuaji wa Mawe (Miamba) zilizokuwa zikifanywa na Kampuni ya Lake Holding katika eneo la Makutano ya Barabara ya Kenyatta na Pamba Jijini Mwanza kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Mafuta.
Na:Binagi Media Group
Eng.Kunyaranyara alichukua hatua hiyo jana ijumaa baada wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo kulalamika kuwa nyumba zao zinapata mipasuko kutokana na milipuko ya baruti zinazotumika kupasulia (miaka) mawe hayo. 

Alisema shughuli za upasuaji wa miamba (mawe) hazipaswi kusababisha athari zozote katika makazi ya watu na hivyo kuondoka na jukumu moja la kwenda kukagua vibali vilivyotolewa kwa kampuni hiyo kwa ajili ya kufanya upasuaji huo na kwamba kama kuna sheria zozote zilikiukwa, Kampuni hiyo itawajibika katika marekebisho yaliyotokea katika makazi ya wananchi.

Baadhi ya wakazi wanaoishi kando ya eneo hilo ambalo lina mwinuko mkali walilalamika nyumba zao kupata nyufa kutokana na baruti japo msimamizi wa Kampuni ya Lake Holding, Halid Faraj alisema kuwa malalamiko hayo yameibuka baada wananchi hao kuomba walipwe fidia ili wapishe katika eneo hilo jambo ambalo halikuwezekana kwa kuwa ujenzi wake hauna athari zozote kwao na kwamba hata baruti anazopiga haziathiri kwa namna yoyote makazi yao.
Mhandisi wa Jiji la Mwanza (Kushoto) akiwa pamoja na Msimamizi wa Kampuni ya Lake Holding (Kulia) wakijionea namna upasuaji wa mawe (Miamba) unavyofanyika. Wananchi wamelalamikia upasuaji huo ambao ni wa kutumia baruti kuwa unaathiri nyumba zao
Malalamiko ya nyumba kupata nyufa kutokana na shughuli za upasuaji mawe zinazofanywa na Kampuni ya Lake Holding
Malalamiko ya nyumba kupata nyufa kutokana na shughuli za upasuaji mawe zinazofanywa na Kampuni ya Lake Holding
Malalamiko ya nyumba kupata nyufa kutokana na shughuli za upasuaji mawe zinazofanywa na Kampuni ya Lake Holding
Mwenye nyumba hii analalamika pia
Kushoto ni Mhandisi wa Jiji la Mwanza Ezekiel Kunyaranyara akiangalia namna upasuaji miamba unavyofanyika
Msimamizi wa Kampuni ya Lake Holding, Halid Falaj (Kulia) akitoa ufafanuzi namna zoezi la upasuaji linavyofanyika katika eneo lake la ujenzi ambapo alieza kuwa hakuna athari zozote zinazojitokeza kwani hata nyufa zilizopo katika baadhi ya nyumba zilizo jirani na eneo hilo ni za siku nyingi.
Eneo likisawazishwa kwa ajili ya ujenzi
Mhandisi Mkuu wa Jiji la Mwanza Ezekiel Kunyaranyara (Katikati) akikagua baadhi ya vibali vya upasuaji wa mawe (Miamba) eneo la barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa milipuko inayofanywa katika eneo hilo inasababisha nyumba zao kupata mipasuko. Kushoto ni Msimamizi wa Kampuni hiyo na kulia ni mtaalamu wa upasuaji miamba.

No comments:

Powered by Blogger.