LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKAMU MKUU WA CHUO CHA USHIRIKA MOSHI ATAKA JAMII KUJIUNGA NA VYAMA VYA USHIRIKA.

Na:Judith Ferdinand, Mwanza
JAMII imeombwa kujiunga  na vyama vya Ushirikka, ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazolikabiri Taifa  ikiwemo  umaskini uliokithiri, ukosefu wa ajira kwa vijana,  huduma za jamii na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Wito huo ulitolewa juzi na  Makamu  Mkuu wa Chuo kikuu cha  Ushirika Moshi ( MoCU), Faustine Bee kwenye Mahafali yaliyofanyika katika uwanja wa chuo hicho tawi la Mwanza.

Bee alisema maendeleo yoyote yanaletwa kwa kushirikiana, hivyo ifike hatua watanzania tutumie fursa ya kujiunga na vyama vya ushirika kwa ajili ya kuchochea uchumi binafsi na wataifa kwa ujumla.

Pia alisema, ili kukuza na kuimarisha  uchumi binafsi na taifa,  ni lazima wananchama na viongozi wapate elimu ya ushirika  ambayo itasaidia kuendesha miradi kitaaluma zaidi.

Aidha alisema, ili jamii ijiunge na vyama hivyo, inatakiwa kupatiwa elimu kuhusu faida ya kujiunga na vyama vya ushirika, kwani kwa kushurikiana, wataweza kumiliki rasilimali za nchi zitakazo wanufaisha wote badala ya kuchukuliwa na makampuni ya nje yanayojali zaidi faida binafsi bila kuangalia wazawa.

Naye Mratibu wa Mipango Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Mwanza, Charles Malunde alisema, mkombozi wa maendeleo ni ushirikiano kwani uwezi leta maendeleo bila ya kuwashirikisha wenzako.

No comments:

Powered by Blogger.