LIVE STREAM ADS

Header Ads

SIKU YA UTALII DUNIANI, JAMII YAHIMIZWA KUWA NA DESTURI YA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII.

Judith  Ferdinand 
Jamii imeombwa kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio mbalimbali, ili kuendeleza utalii wa ndani, kujifunza na kijionea jinsi Tanzania ilivyobarikiwa katika suala zima la maliasili.

Hii ni kutokana na watanzania kutokuwa na mwiitikio wa kutembelea vivutio vya utalii vilivopo ndani ya nchi, licha ya wadau mbalimbali kuhamasisha na kutoa elimu.

Wito huo ulitolewa  jana na Afisa Mfawidhi Bodi ya Utalii Kanda ya Ziwa Gladstone Mlay, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya utalii dunia iliyofanyika kwa Mkoa wa Mwanza katika uwanja wa Kamanga Ferry (Rock Bismark).

“Watanzania utalii ni sisi, ili kuhamasisha watalii kutoka nje tunatakiwa kujenga utamaduni wa kutembelea na kutunza vivutio tulivyo mbarikiwa na Mungu, kwa ajili ya kuendeleza pato la taifa na binafsi,” alisema Mlay. 

Mlay alisema, utalii ni sehemu ya maisha  jamii inalojukumu la kutembelea na kutunza vivutio hivyo, ili kujifunza mambo yaliyofanyika kale kwa uhalisia, sambamba na kufanya utafiti.

Hata hivyo aliwaomba wananchi mkoani hapa, kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo yalioanza kufanyika Novemba 25  na kufikia tamati tarehe 29 mwezi huu kwani hakuna kiingilio, ili kupata elimu juu ya masuala ya utalii na kujionea wanyama mbalimbali.

Pia alisema, ili kuendeleza utalii wa ndani  ni wajibu wa kila mmoja ikewemo Serikali, taasisi  na kampuni binafsi kuelimisha  na  kuhamasisha jamii kupitia  vyombo vya habari, matamasha na semina.

No comments:

Powered by Blogger.