TRA MKOANI KAGERA YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MASHINE ZA EFD'S.
Na:Anatory Elisa,Kagera
Mamlaka ya Mapato TRA Mkoani Kagera imekiri kuwa na upungufu wa Mashine za kutolea risiti za EFD's zipatazo 1,700 jambo linalosababisha mamlaka hiyo kutokusanya mapato ya kutosha.
Hayo yalibainishwa jana na Apil Mbarouk ambae ni Meneja wa mamlaka hiyo Mkoani humo, wakati akizungumza na mwanahabari wetu.
Alisema hadi sasa Mamlaka hiyo ina mashine 334 ambazo hazikidhi mahitaji mahitaji ya wafanyabiashara Mkoani humo.
Aidha Mbarouk aliwatahadharisha baadhi ya wafanyabiashara ambao hawajaanza kutumia mashine hizo za EFD's kuanza kufanya utaratibu wa kuziagiza ili waanze kuzitumia maana mamlaka hiyo inatarajia kufanya ukaguzi ili kubaini wanaokwepa kuzitumia na kuwachukulia hatua za kisheria.
Hata hivo baadhi baadhi ya wafanyabiashara Mkoani Kagera wameilalamikia Mamlaka hiyo kutokana na kudai kuwa mashine za EFD's zinaharibika mara kwa mara na hivyo kuwasababishia hasara ambapo wameiomba serikali kuendelea kushughulikia matatizo ya mashine hizo.

No comments: